August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Odinga, Ruto wakabana koo uchaguzi mkuu Kenya

Raila Odinga

Spread the love

 

VINARA wa kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu nchini Kenya, Raila Odinga wa Azimio na Dk. Wiliam Ruto wa Kenya Kwanza kimezidi kushika kasi baada ya kura mpya za maoni za Shirika la utafiti la Tifa lenye makao yake jijini Nairobi, kuonyesha kuwa wawili hao wako sawa ki-takwimu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Odinga ambaye ni kiongozi wa upinzani anayewania nafasi hiyo kwa mara ya tano anaongoza kwa asilimia 46.7 na mpinzani wake Ruto ambaye ni naibu rais wa sasa ana asilimia 44.4 ya kura.

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ili kushinda katika duru ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu, mgombea anahitaji zaidi ya nusu ya kura zote angalau asilimia 25 ya kura zilizopigwa katika majimbo takriban nusu miongoni mwa yote 47.

Dk. Wiliam Ruto

Ikilinganishwa na kura za maoni za awali za utafiti wa Tifa, sasa zinaonyesha kuwa kura za Ruto zimepungua dhidi ya Odinga ambaye awali alikuwa na asilimia 42 dhidi ya asilimia 39 za Ruto.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa Odinga ana uungwaji mkono zaidi katika maeneo ya Nyanza, magharibi ya Kusini ya Rift, Nairobi na sehemu za Lower Eastern, wakati Ruto ana uungwaji mkono zaidi katika maeneo ya kati ya Rift na Mlima Kenya.

error: Content is protected !!