August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jafo aagiza Dodoma kununua vifaa vya usafi

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kutenga fedha kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya usafi hususani katika Soko la Bonanza. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Jafo ametoa agizo hilo leo tarehe 30 Julai,  2022 alipokuwa akizungumzia na wafanyabiashara wa Matunda na mbogamboga na wauza samaki muda mfupi baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika soko hilo jijini Dodoma.

Pia amewahimiza watanzania kuwa na desturi ya kufanya usafi bila kusukumwa na kuwakumbusha kujitokeza kuhesabiwa wakati wa sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti mwaka huu.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na Mkuu wa Idara ya utunzaji mazingira na taka ngumu, Dickson Kimaro amesema kuwa Halmashsuri ya Jiji la Dodoma katika mwaka wa bajeti 2022/23 imetenga Sh. milioni 38 kwa ajili ya kuboresha soko la Bonanza.

Aidha, Kimaro amesema  jiji la Dodoma limekuwa na kauli mbiu ya usafi ambayo inasema “mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano”.

Ameongeza kuwa katika mapambano ya usafi kila Jumamosi ufanyika usafi katika maeneo mbalimbali isipokuwa Jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni Jumamosi ya mazoezi.

Nao mabalozi wa mazingira ambayo walioratibu zoezi hilo wamesema kuwa suala la mazingira ni la kila mmoja badala ya kusubiri kuimizwa.

Mmoja wa Mabalozi wa Mazingira, Sakina Abdulah Masoud ambaye ni mwandishi wa radio Uhuru amesema kuna faida kubwa ya kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kusababisha afya kuwa njema.

Pia amehimiza jamii kutunza mazingira pamoja na upandaji wa miti ya matunda na kivuli.

error: Content is protected !!