Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Odinga ‘achekelea’ demokrasia ya Ghana
Kimataifa

Odinga ‘achekelea’ demokrasia ya Ghana

Wananchi wa Ghana wakipiga kura
Spread the love

RAILA Odinga Kiongozi wa Muungano wa Upinzani wa CORD na miongoni mwa watu mashuhuri kutoka Afrika Mashariki watakaohudhuria kuapishwa kwa Nana Akufo Addo rais mteule wa Ghana tarehe 7 Januari mwaka huu, amepongeza kukua kwa demokrasia nchini Ghana, anaandika Wolfram Mwalongo.

Odinga ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya chini ya Rais Mwai Kibaki, amempongeza Rais John Mahama wa Ghana kwa kuheshimu demokrasia kwa kukubali kushindwa katika uchaguzi akisema, “ni mfano wa kuigwa na abara zima la Afrika.”

Odinga ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwa safarini kuelekea Ghana kushiriki sherehe hiyo itakayohudhuriwa na viongozi zaidi ya 6,000 kutoka mataifa tofauti tofauti.

Odinga ameambatana na Hassan Ali Joho, makamu wake ndani ya chama cha Orange For Democratic Movement (ODM) ambaye pia ni Gavana wa Kaunti ya Mombasa.

Sherehe hizo zifanyika jijini Accra katika viwanja vya Uhuru, ambapo Nana Akufo Addo ataapishwa rasmi tayari kwakushika hatamu ya kuongoza nchi ya Ghana baada ya kutangazwa mshindi huku Rais Mahama akiridhia kushindwa.

“Nimekubali kushindwa kuwa kuwa aliyeshinda ni Mghana mwenzetu,” alisema Rais Mahama katika hotuba iliyopongezwa na wengi.

Aidha, Mahama pia aliwapongeza wananchi wote wa Ghana kwa kutumia vyema haki yao ya kidemokrasia na kumchagua Kiongozi huyo wa Upinzani huku akiahidi kuendelea kushirikiana na serikali hiyo mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!