Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyetumwa kumtukana Nchimbi ajisalimisha
Habari za SiasaTangulizi

Aliyetumwa kumtukana Nchimbi ajisalimisha

James Mwakibinga
Spread the love

IKIWA ni zaidi ya miezi minne tangu James Rock Mwakibinga, kada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kumtuhumu Dk. Emmanuel Nchimbi kuhusika na ufisadi mkubwa ndani ya chama hicho, hatimaye ameomba radhi, akijutia kitendo hicho, anaandika mwandishi wetu.

Mwakibinga alimtuhumu Dk. Nchimbi kuhusika na uuzaji wa viwanja zaidi ya 200 mali ya UVCCM, vilivyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam huku akiwambia wanahabari kuwa ana ushahidi wa ufisadi huo na kwamba angeutoa iwapo muhusika angejitokeza kukanusha.

“Kuna mtandao wa wezi na wabadhirifu wa mali za UVCCM unaofanywa na vijana pamoja na baadhi ya watendaji, na ujangili huu unaaanzia katika Baraza la Wadhamini la Vijana chini ya Dk. Emmanuel Nchimbi,” alidai Mwakibinga.

Siku saba baadaye Dk. Nchimbi kupitia mawakili wake (FK Law chambers) alimtaka kijana huyo kuthibitisha madai hayo ndani ya siku saba au kuomba radhi na kulipa fidia ya Sh. 2.5 bilioni la sivyo, angemfikisha mahakamani.

“Tumeelezwa na mteja wetu kwamba, uchukue kila hatua itakayosafisha jina lake kwa kuitisha mkutano mwingine na wanahabari mara moja na ukanushe tuhuma ulizotoa na kuomba radhi.

“Pia ufute na kuondoa taarifa iliyomkashifu katika vyombo vyote vya habari pamoja na mitandao ya kijamii na umlipe haraka iwezekanavyo mteja wetu fidia ya shilingi 2.5 bilioni,” ilisema sehemu ya barua ya mawakili wa Dk. Nchimbi.

Akiitikia amri ya kuomba radhi, hii leo Mwakibinga amesema katika taarifa yake kwa umma;
“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Umoja wa Vijana Makao Makuu haujawahi kumiliki viwanja katika eneo lolote la Temeke na hivyo madai kuwa Dk. Nchimbi ameuza viwanja 200 hayana ukweli wowote.”

Amedai kuwa hapo awali alipata taarifa hizo kutoka chanzo kisicho rasmi na kuziamini kabla ya kuutangazia umma akidhani kitendo hicho ni cha kizalendo hata hivyo alipotakiwa kuthibitisha alitafuta ushahidi na kushindwa kuupata.

Kauli ya leo ya Mwakibinga ni tofauti na ile ya tarehe 16 Agosti, 2016 alipodai mbele ya wanahabari kuwa anao ushahidi wa ufisadi huo na kuonesha mkoba aliokuwa nao akisema ndiyo umebeba ushahidi huo na kwamba angeweka wazi iwapo Dk. Nchimbi atakanusha.

Kushambuliwa kwa Dk. Nchimbi kupitia kijana huyu kabla ya kuombwa radhi leo, ni muendelezo wa siasa za visasi ndani ya CCM na kwamba zipo dalili za wazi kuwa Mwakibinga alitumiwa na vigogo au kigogo mwingine ndani ya chama hicho ili kumchafua mwanasiasa huyo.

Kuombwa radhi kwa Dk. Nchimbi pia kunakuja ikiwa mwezi mmoja tangu Rais John Magufuli amteue mwanasiasa huyo kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ambayo bado haijatajwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

error: Content is protected !!