Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ntakarutima wa Burundi Spika mpya EALA
Kimataifa

Ntakarutima wa Burundi Spika mpya EALA

Joseph Ntakarutimana
Spread the love

 

HATIMAYE Joseph Ntakarutimana kutoka nchini Burundi ameshaguliwa na Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), kuwa Spika wa bunge hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ntakarutimana ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Burundi cha (CNDD-FDD) amechaguliwa katika uchaguzi uliofanyila leo Desemba 20 mjini Arusha na kuchukua nafasi ya aliyekuwa spika wa zamani, Martin Ngoga kutoka nchini Rwanda.

Spika huyo alikuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya wagombea wawili kutoka nchini Sudani Kusini, Gai Deng na Dk Anne Itto kujitoa dakika za mwisho na hivyo kusababisha mgombea huyo kukosa ushindani.

Akisimamia uchaguzi huo, Katibu wa Bunge la EALA, Alex Obatre ametoa nafasi kwa wagombea hao waliojitoa kutamka kwa vinywa vyao kuwa wamejitoa, baada ya kuwasilisha taarifa rasmi ya kujitoa, ambapo wamesimama na kusema wana muunga mkono mpinzani wao.

Katika upigaji kura Spika huyo mpya amepata kura za ndiyo 54 kati ya kura 63 za wabunge  wote kutoka nchi saba za EAC, ambapo kura nane ziliharibika na kura moja haikupigwa kabisa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!