Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Habari za kuiwajibisha Serikali nadra – Utafiti
Habari Mchanganyiko

Habari za kuiwajibisha Serikali nadra – Utafiti

Spread the love

 

KIWANGO cha uandishi unaochagiza uwajibikaji nchini Tanzania kinapanda taratibu mno huku magazeti yakijitutumua kwenye eneo la kuwapa haki ya kusema wale wanaotuhumiwa. Anaripoti Jabir Idrissa
Zanzibar … (endelea).

Ripoti ya hali ya ubora wa uandishi ya mwaka huu wa 2022 iliyozinduliwa hivi karibuni inaonesha kuwa katika habari zilizofanyiwa kazi kwenye utafiti, ni asilimia 40 tu watuhumiwa walipewa nafasi ya kutoa msimamo juu ya wanachohusishwa kutenda, kiwango cha juu kidogo ingawa kimepita kile cha mwaka 2019.

Huu ndio ugunduzi wa watafiti uliotangazwa na Dk. Abdallah Katunzi ambaye ni mmoja wa watafiti wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma iliyo sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (SJMC-UDSM), kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip, mjini hapa.

Mbele ya Wahariri, Wadau wa Habari na Mabalozi wa Uholanzi na Uswisi, Dk. Katunzi alisema uandishi mzuri ni ule unaotoa habari na makala zilizoshiba vyanzo na zinazolenga kuelekeza ufumbuzi wa matatizo; habari zilizojumuisha mitizamo ya vyanzo tofauti na zisizoegemea upande mmoja tu wa kutuhumu.

“Utoaji habari wa kiwango hichi unahitaji dhamira, umahiri na utiifu kwa maadili ya kitaaluma. Habari hizi ni chache kuliko ilivyokuwa hapo nyuma,” alisema Dk. Katunzi.

Akigusa eneo tete la kuikosoa serikali chini ya dhamira ya kuchagiza utawala bora na uwajibikaji, alisema utafiti huu umetanua wigo zaidi ya kuilenga tu serikali na taasisi zake kwa habari zinazoihusu. Utafiti umegusa habari zilizohusu sekta binafsi, asasi za kiraia na hata taasisi za kidini ambako “imeonesha ni asilimia 4 tu ya habari zilizotafitiwa ndio zimekosoa (kwa muelekeo wa kuchagiza uwajibikaji) serikali.”

Ripoti ambayo pia uzinduzi wake ulishuhudiwa na Waziri wa Habari wa Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, inaonesha kati ya habari 147 zilizochambuliwa kulenga kukosoa, ni asilimia 3.9 tu ziliigusa Serikali.

Kwa jumla, utafiti huo wa ubora wa maudhui uliohusu vyombo vya habaru vya Tanzania na Zanzibar – magazeti, televisheni na redio – umebaini kuwepo ongezeko kubwa la habari zinazohusu matukio kuliko zile zilizotokana na uchunguzi wa kina ambazo ndio hasa huazimiwa kuchagiza uwajibikaji serikalini au kwengineko.

Hali hii ya kupungua kwa habari za kukosoa serikali katika azma ya kuihimiza kuwajibika kwa raslimali za umma na matumizi mazuri ya ofisi, Naibu Waziri wa Elimu na MafuNo ya Ufundi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abdulgulam Hussein alisikitika kuwa mtindo huo unazorotesha kuonesha mchango muhimu wa vyombo vya habari kwa taifa.

Naibu Waziri Abdulgulam alihimiza mabadiliko kwa vyombo vya habari kuchukua jukumu lao hilo kwa weledi na ujasiri ili kuthibitisha vilivyo mhimili wa nne wa dola baada ya Utawala, Mahkama na Bunge.

Mabalozi waliahidi kuendelea kusaidia shughuli ya utafiti inaulyofanywa na Skuli Kuu ya Uandishi wa Habari kwa kuamini hatua yao inasaidia kukuza upeo wa uhuru wa kujieleza na haki ya wananchi kupata taarifa. Ufadhili wao umeendelea kwa mwaka wa tatu tangu utafiti huo ulipoanza rasmi mwaka 2018.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!