SERIKALI ya Tanzania imeombwa kuongeza bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, ili zitekeleze majukumu yake ya ufanisi katika kutatua migigoro kati ya wakulima na wafugaji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Wito huo umetolewa peo Jumanne, tarehe 20 Desemba 2022 na mashirika sita yasiyo ya kiserikali (NGO’s), likiwemo la Haki Ardhi, Tanzania Land Alliance na Pingo’s Forum.
Katika tamko la pamoja la taasisi hizo, zimesema ongezeko la bajeti hizo litasaidia ubainishwaji na upimaji wa nyanda za malisho ya wafugaji, na maeneo ya kilimo.
“Bajeti ziongezwe kwa ajili ya ubainishaji na upimaji wa nyanda za malisho, kauli za kutaka mamlaka hizo kutekeleza wajibu wake bila kuziwezesha ni kiini macho na mwendelezo wa matamko yasiyotekelezeka,” imesema tamko la taasisi hizo.
Katika hatua nyingine, taasiai hizo zimeiomba Serikali ianzishe mijadala ya wazi ya wananchi Ili kutafuta suluhisho la migogoro ya ardhi na uhifadhi.
Mashirika yametoa apendekezo hayo yakisema migogoro ya ardhi imeongezeka ambapo wakulima na wafugaji wameathirika nayo hususan wenye mifugo ambao wamepata hasara baada ya kupigwa mnada kwa makosa ya kuingia maeneo yasiyo sahihi Kwa ajili ya malisho.
Leave a comment