Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yazindua bima ya wavuvi, Waziri Ndaki atoa wito
Habari Mchanganyiko

NMB yazindua bima ya wavuvi, Waziri Ndaki atoa wito

Spread the love

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wavuvi nchini kuchangamkia bima maalum ijulikanayo kama Jahazi, ili iwasaidie kuwakinga wanapokumbwa na majanga mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Ndaki alisema hayo jana Jumapili, tarehe 31 Oktoba 2021, jijini Mwanza, wakati Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Britam kuzindua bima hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi katika mikoa mbalimbali nchini.

Alisema siku za nyuma bima ilikuwa inawaangalia wavuvi wakubwa pekee na kwamba kwa sasa NMB na Britam wamekuja na aina mpya ya kuwasaidia wavuvi wadogo na wa kati.

Aliwataka wavuvi waendelee kupewa elimu ya bima ili waijue na kufanya uamuzi kwa kuwa ni njia sahihi ya kuwasaidia katika kipindi chote wanapokuwa katika shughuli zao.

Alisema benki hiyo imedhamiria kuwainua kiuchumi wakulima, wafugaji na sasa ni zamu ya wavuvi na kwamba serikali inatambua mchango wao katika kuhakikisha makundi hayo yananufaika na mikopo inayotolewa na benki hiyo.

Alisema sekta ambazo zilikuwa zinaonekana kuwa na ‘risk’ kwa sasa zianze kufikiwa na kukatiwa bima kwa kuwa zina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.

Waziri Ndaki alisema sekta ya uvuvi inaajiri watu milioni 4.5 na kwamba inachangia asilimia 1.7 ya pato la taifa hivyo ni kundi muhimu ambalo linatakiwa kusaidiwa ili liweze kupiga hatua.

Awali, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi aliserma bima hiyo inawalenga wavuvi wadogo na wa kati hapa nchini.

Alisema wavuvi watakata bima ya asimilia 3 ya chombo husika cha shughuli ya uvuvi na kwamba wataweza kukingwa na majanga ya ajali, kuungua mitumbwi ama boti pamoja na watu watakaokuwa ndani ya vyombo hivyo.

Mponzi alisema faida nyingine za bima hiyo ni pamoja na familia ya mvuvi ama mtu aliyekuwa ndani ya chombo hicho kupewa mkono wa pole endapo kutatokea kifo pamoja na kupata ulemavu wa kudumu.

Aidha, bima hiyo itatoa gharama za matibabu kwa mvuvi pamoja na kulipwa fidia kutokana na ajali yoyote itakayompata atakapokuwa majini kwa ajili ya shughuli za uvuvi ama kando kando ya ziwa, mto, bwawa ama bahari.

Mponzi aliwataka wavuvi kufika katika ofisi za NMB kwa ajili ya kukata bima ambayo itawakinga na majanga mbalimbali wanapokuwa katika shughuli zao kwenye maziwa, mito, mabwawa na bahari.

Kwa upande wake, Meneja wa kampuni ya Bima ya Britam kanda ya ziwa, Said Kadabi alisema bima hiyo itawasaidia wavuvi katika kuinuka kiuchumi kwa kuwa sasa watanya kazi zao kwa kujiamini.

Alisema wanalenga kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii na kuyakatia bima ikiwamo mama lishe ili waweze kufanya shughuli zao kwa kujiamini zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!