Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Megawati 700 za nishati jadidifu kuzalishwa 2024
Habari Mchanganyiko

Megawati 700 za nishati jadidifu kuzalishwa 2024

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felischemi Mramba akizungumza wakati wa ufungaji wa warsha iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini kuhusu nishati jadidifu
Spread the love

 

KATIKA kukabiliana na changamoto ya umeme nchini Serikali imesema itashirikiana na wawekezaji kuzalisha megawati 700 za nishati jadidifu ifikapo mwaka 2024. Anaripoti Selemani Msuya, Bagamoyo … (endelea)

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Felschemi Mramba wakati akifunga warsha ya siku tano kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini na kufanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema analipongeza Shirika la HakiMadini kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ambao ni watu muhimu kwenye kutoa elimu kuhusu nishati jadidifu.

Mramba Serikali kupitia Wizara ya Nishati imepanga kutekelezaji maalekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa siku akihutubia Bunge kuwa hadi 2025 wawe wamezalisha megawati 1,100 za nishati jadidifu.

“Ndugu zangu wana habari naamini mafunzo haya ymekuwa na mchango mkubwa kwenu, kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuzalisha megawati 500 za umeme jua na upepo ifikapo 2023, lakini pia Kampuni yetu ya Jotoardhi inatarajia kuzalisha megawati 200 hivyo tutakuwa na megawati 700 za nishati jadidifu ifikapo 2024 ,” alisema.

Kamishna Mramba alisema kuanzia mwaka 2023 hadi 2025 wanatarajia kuongeza megawati zingine 400 hivyo lengo la kufikia megawati 1,100 litafanikiwa na kuwa na umeme wa uhakika kwa nchi.

Mtaalam huyo wa masuala ya umeme alisema sababu ya Serikali kuwekeza megawati chache ni kutokana na uwezo wa gridi ya taifa ambayo inahitaji megawati chache hivyo wataendelea kuwekeza hatua kwa hatua kwa kuboresha gridi.

“Tunaendelea kuzungumza na wawekezaji kuja kuwekeza katika nishati jadidifu kwa kuwa ni nishati inayohitajika kwa sasa kutokana na ubora wake katika utunzaji mazingira na endelevu,” alisema.

Alisema Serikali imejipanga kutatua changamoto za kisera na sheria ili kuvutia waeekezaji kuwekeza kwenye nishati jadidifu.

Kamishna Mramba alisema umeme unaozalishwa kwa njia nishati jadidifu utauzwa kwa Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mramba alisema utafiti uliofanywa unaonesha nishati jadidifu hasa ya umeme jua na upepo inapatikana kwenye mikoa ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Singida, Shinyanga, Iringa, Njombe na Mbeya hivyo kuwaomba wawekezaji kuja kuwekeza maeneo hayo.

Alisema umeme wa Jotoardhi unapatikana katika eneo lote la bonde la ufa na kwamba kwa siku zijazo hizo ndio zitakuwa nishati muhimu kwenye uchumi na maendeleo nchini.

Halikadhalika alisema pia Tanzania inafursa ya umeme wa mawimbi ambao unaweza kuzalishwa baharini na kwamba kinachohitajika ni uwekezaji.

Alisema kwa sasa gridi ya taifa ina megawati 1,605 na kwamba iwapo megawati 1,100 za nishati jadidifu zikipatikana na megawati 2,115 zinazozalishwa kwenye Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) Tanzania itakuwa salama kwenye nishati na utunzaji wa mazingira.

Alisema mikakati yao ni kuhakikisha mikoa yote ambayo haipo kwenye gridi ya Taifa kama Kigoma, Katavi, Rukwa na wilaya za Mafia na Longido zinaingia kwenye gridi ya taifa.

Kamishna alisema kwa sasa gridi ya taifa ina umeme wa gesi megawati 900, maji megawati 508 na nishati jadidifu megawati 58 na mafuta megawati 139.

Naye Mjumbe wa Bodi wa Shirika la HakiMadini alisema wamelazimika kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini ili wawe na uelewa kuhusu nishati jadidifu ambayo ni fursa muhimu kwa uchumi na maendeleo ya jamii.

“Mafunzo haya ni muhimu kwa kundi hili, imani yetu sisi HakiMadini ni kuona wakiandika habari hizi ili kuelimisha na kuvutia wawekezaji kuhusu fursa hii iliyopo nchini,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!