Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shahidi wa Jamhuri asimulia wenzie Mbowe walivyokamatwa 
Habari za SiasaTangulizi

Shahidi wa Jamhuri asimulia wenzie Mbowe walivyokamatwa 

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na wenzake wakiwa mahakamani
Spread the love

 

SHAHIDI wa nne wa Jumhuri, Anita Varelian Mtaro (45), mfanyabiashara wa kuuza mbege, Rau Madukani mkoani Kilimanjaro ameelezea jinsi Adam Kasekwa na Mohamed Abdillah Ling’wenya walivyokamatwa wakiwa na silaha aina ya bastola na dawa za kulevya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Anita ametoa ushahidi huo leo Jumatatu, tarehe 1 Novemba 2021, Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joackim Tiganga.

Wawili hao ni miongoni mwa watuhumiwa wanne akiwemo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha Chadena, Freeman Mbowe wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi mahakamani hapo.

Mbali na hao kwenye kesi hiyo, mwingine ni Halfan Hassan Bwire.

Anita ametia ushahidi wake akiongozwa na Wakili Serikali Esther Martin ambapo ameelezea tukio zima lilivyokuwa tarehe 5 Agosti 2020 la kukamatwa kwa Kasekwa na Ling’wenya kisha kufikishwa Kituo Kuu cha Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mahojiano hayo yalikuwa hivi;

Wakili wa Serikali: Mbali na Biashara yako ya Mbege unabishara gani Nyingine

Shahidi: Kuna Glocery, Stationary, banda la tigo pesa na kuna sehemu ya kutolea muvi

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama tarehe 05 Agosti 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Sehemu yangu ya Biashara Nikifanya Usafi

Wakili wa Serikali: Saa ngapi

Shahidi: Saa saba kasoro mchana

Wakili wa Serikali: Kabla ya kufika eneo lako la biashara ulikuwa umetoka wapi

Shahidi: Nilikuwa nimetoka nyumbani nikaenda saloon Kuosha nywele

Wakili wa Serikali: Na ulipotoka saloon kuelekea sehemu yako kufanya usafi ulikuta nini?

Shahidi: Nilikuta wakaka watatu walikuwa wamekaa mbele yangu walikuwa wanakunywa na kusajili laini.

Wakili wa Serikali: Walikuwa wanakunywa nini

Shahidi: Walikuwa wanakunywa bia

Wakili wa Serikali: Ukiwa unafanya usafi kitu gani kingine ulishuhudia

Shahidi: Kuna wakaka wawili walikuwa wanapitapita wakiongea na simu. Wanaenda wanarudi wakiongea na simu.

Wakili wa Serikali: Hao wanaopita ni tofauti na wale uliposema walikuwa wanakunywa bia

Shahidi: Hapana ni walewale.

Wakili wa Serikali: Kutoka kwako unapofanyia kazi mpaka glocery ni umbali gani.

Shahidi: Kama hatua 10.

Wakili wa Serikali: Hapo katikati sasa kati ya glocery na ulipo pana kitu gani

Shahidi: Pana uwazi.

Wakili wa Serikali: Baada ya muda kitu gani kilitokea.

Shahidi: Wakati wanaongea na simu walitokea watu wawili wa kaongea kwa sauti kali “mpo chini ya ulinzi mnahusika na mambo ya kigaidi, chuchumaa chini mikono juu.”

Wakili wa Serikali: Kitu gani kingine ulisikia.

Shahidi: Ni Askari.

Wakili wa Serikali: Ni watu gani sasa hao.

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unafanya nini wakati huo.

Shahidi: Nafanya Usafi.

Wakili wa Serikali: Pana umbali gani kutoka walipo mpaka ulipokuwa unafanya usafi.

Shahidi: Hatua tano.

Shahidi: Sikusikia kingine zaidi ya chuchumaa chini nyoosha mikono juu.

Wakili wa Serikali: Ukisikia nini kingine.

Wakili wa Serikali: Walikuwa askari wangapi.

Shahidi: Wawili.

Wakili wa Serikali: Hali ya pale ilikuwaje.

Shahidi: Ilikuwa ni utulivu.

Wakili wa Serikali: Nini kilifuata.

Shahidi: Walitokea askari wengine watatu wakawa wamefika eneo la tukio.

Wakili wa Serikali: Ongeza sauti. Kitu gani Kiliendelea.

Shahidi: Baada ya kuwa askari watano alitokea mmoja akaniambia anaomba nisogee anahitaji kuwafanyia upekuzi.

Wakili wa Serikali: Ni askari gani huyo.

Shahidi: Alinitambulisha anaitwa Askari Polisi Jumanne.

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini kujiridhisha.

Shahidi: Alitoa kitambulisho akanionesha.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo nini kilifanyika.

Shahidi: A.limsimamisha mmoja.

Wakili wa Serikali: Kabla ya kumsimamisha..?

Shahidi: Afande Jumanne alijipekua kuanzia kifuani akatoa mifuko nje.

Wakili wa Serikali: We ulikuwa na nani wakati huo.

Shahidi: Dada mmoja anaitwa Esther.

Wakili wa Serikali: Kutoka eneo la walioambiwa wachuchumae chini, palikuwa na umbali gani.

Shahidi: Kama hatua mbili.

Wakili wa Serikali: Kuna kitu gani kingine.

Shahidi: Raia walikuwa wamekuja.

Wakili wa Serikali: Kabla ya raia kusogea eneo hilo palikuwa na hali gani. Na nini kiliendelea.

Shahidi: Alimsimamisha mmoja akamuuliza unaitwa nani.

Shahidi: Adam Kasekwa.

Wakili wa Serikali: Akamwambia nini.

Shahidi: Akiwa amenyoosha mikono juu akamwambia geuka, akageuka.

Wakili wa Serikali: Baada ya kugeuka.

Shahidi: Askari Jumanne alianza kumpekua kuanzia kichwani, mabegani, alipofika kiunoni alikuta kitu kigumu.

Wakili wa Serikali: Alikikuta upande gani.

Shahidi: Kushoto.

Wakili wa Serikali: Maeneo gani.

Shahidi: Niliona ni Bastola.

Wakili wa Serikali: Ulijuaje kama ni Bastola.

Shahidi: Afande Jummane alituambia ni Bastola.

Wakili wa Serikali: Halafu.

Shahidi: Akatuonyesha namba.

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni namba gani?

Shahidi: A5340.

Wakili wa Serikali: Wakati anakuonyesha Bastola Adam alikuwa wapi.

Shahidi: Alikuwa amesimama.

Wakili wa Serikali: Uliona na nini kingine.

Shahid:i Risasi 03.

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea.

Shahidi: Akaendelea na upekuzi. Alipofika upande wa kulia akakuta vitu vidogo vidogo kwenye karatasi ya nailon akasema inasadikiwa na dawa za kulevya ila itajulikana mbele.

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ngapi, ikawaje.

Shahidi: 58. Aliendelea kumpekua akamkuta na simu ndogo aina ya Itel.

Wakili wa Serikali: Hiyo simu akaifanyeje.

Shahidi: Akatoa laini akakuta namba akaziandika.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo aliendelea na nini.

Shahidi: Akamwambia naomba fomu, akaleta fomu.

Wakili wa Serikali: Fomu ngapi.

Shahidi: Zilikuwa mbili.

Wakili wa Serikali: Akafamya nini sasa kwenye ile fomu.

Shahidi: Akaandika vitu alivyokuwa amempekua.

Wakili wa Serikali: Umesema palikuwa na fomu mbili, fomu ya kwanza alijaza nini.

Shahidi: Fomu ya kwanza alijaza bastola, risasi na laini. Slipo maliza kujaza akampa akasaini na baadae akasaini yeye alipo maliza kusaini.

Wakili wa Serikali: Alimpa nani.

Shahidi: Alimpa Adam.

Wakili wa Serikali: Baada kumalizia nini kilifuata.

Shahidi: Akamuita mwingine, Mohamed Abdulahi Ling’wenya, asimame ageuke na baada ya kugeuka akaanza kumpekua. Upande wa Kulia alikuta na vikete vidogo vidogo 25.

Wakili wa Serikali: Alikuta vitu gani pia.

Shahidi: Alikuta simu aina ya Techno nyeusi na baada ya upekuzi akaomba fomu mbili akazijaza na kuzisaini.

Wakili wa Serikali: Baada ya upekuzi.

Shahidi: Walivalishwa pingu.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo.

Shahidi: Afande Jumanne akatuomba tuelekee kituoni.

Wakili wa Serikali: Hao walivalishwa Pingu walikuwa ni akina nani.

Shahidi: Adam na Mohamed.

Wakili wa Serikali: Sasa baada ya kumalizia mkaelekea kituoni, kituo gani?

Shahidi: Central Moshi na tulipofika tuliandika maelezo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kujua kinachoendelea kwani kwa sasa anahojiwa na upande wa utetezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!