Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Saini ya shahidi yaibua mvutano kesi ya Mbowe, yaahairishwa
Habari za SiasaTangulizi

Saini ya shahidi yaibua mvutano kesi ya Mbowe, yaahairishwa

Spread the love

 

USAHIHI wa saini ya shahidi wa nne wa Jamhuri, Anita Varelian Mtaro (45), mfanyabiashara wa kuuza mbege, katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake, umeibua mvutano na kusababisha Jaji Joackim Tiganga kuahirisha kwa dakika 10. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo wengine ni, Adam Kasekwa, Mohamed Abdillah Ling’wenya na Halfan Hassan Bwire wanaotuhumiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanga njama ya vitendo vya rushwa.

Mvutano huo umeibuka leo Jumatatu, tarehe 1 Novemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mara baada ya Anita kuanza kuhojiwa na upande wa utetezi.

Ni baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, akiongozwa na Wakili wa Serikali, Esther Martin ambapo ameelezea jinsi Kasekwa na mwenzake Ling’wenya walivyokamatwa na askari polisi Rau Madukani, mkoani Kilimanjaro mchana wa tarehe 5 Agosti 2021.

Katika ushahidi wake, Anita alidai Kasekwa baada ya kupekuliwa akikutwa na silaha aina ya bastola, risasi tatu na dawa za kulevya kete 58 na simu huku Linyw’enya alikutwa na dawa za kulevya kete 25 pamoja na simu.

Shahidi huyo alidai, polisi walijaza fomu mbili mbili kwa kila mmoja kutokana na vitu walivyokanamatwa navyo nay eye alikuwa miongoni mwa waliosaini fomu hizo kama shahidi aliyeshuhudia ukamataji na upepuaki akiwa na mwenzake aliyemwita Da Esther.

Mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi na vilelezo vya maelezo yake kupokelewa mahakamani, uliwadia wasaaa wa upande wa utetezi kumhoji akianza Wakili Jeremiah Mtobesya kutaka shahidi huyo asaini sehemu nyingine ili kupata mlinganisho.

Hatua hiyo iliibua mvutano baina yake, mawakili wa utetezi, Jaji mwenyewe pamoja na mawakili wenzake wa utetezi Nashon Nkungu na John Mallya.

Mvutano huo uliosababisha Jaji kuisimamisha kesi kwa dakika 10 ulianza hivi; 

Mtobesya: Naomba Nipatiwe ID 1. Mahakama inampatia

Mtobesya: Shahidi umeomba Mahakama ipokee kielelezo hiki. Onesha sehemu ipo saini

Shahidi: Nimesaini hapa

Mtobesya: Kwa ushahidi wako unasema ulisaini nyaraka ngapi

Shahidi: Nne

Mtobesya: Naomba kwa kifungu 75(1), Sheria ya Ushahidi, shahidi asaini tena sehemu nyingine ili Mahakama iweze kufananisha saini zake na ushahidi wako kwamba sahihi zako zote zinafanana

Jaji: Unaweza Kutusomea? Hicho  kifungu kinaitaka Mahakama shahidi asaini ili iweze kufanya ufafananisho

Mtobesya: Anasoma Kifungu cha 75(1) cha Sheria ya Ushahidi. Ndiyo ili  Mahakama iweze kufananisha, kwa sababu tuna nyaraka nyingine inasaini yake tofauti

Jaji: Lakini hiyo nyaraka itakuwa imetengenezwa hapa

Jaji: Bwana Matata unajambo la ku-she na sisi. Labda utumie hiyo nyaraka nyingine kama upande wa pili watatu Object tutaona

Matata: Sheria anayosoma Wakili Mtobesya ni sheria inasema shahidi anaweza kuandika sehemu tu 75(2) Mahakama inaweza Kuagiza mtu yoyote mahakamani kulingananisha

Jaji: Je hiyo inahusiana na Mahakama kumuelekeza shahidi asaini

Wakili Mallya: Pale kwenye 75(2), inasema any documents aijambana wapi kwa hiyo anaweza kusaini popote (any documents) ili Mahakama ifanye uamuzi iwe imepata kwa usahihi wake

Jaji: upande wa mashitaka

Wakili wa Serikali: Maombi ya Mtobesya pamoja na kuegemea kutoka kifungu 75 cha Sheria ya Ushahidi, tunaona amekimbia sana na siyo wakati wake.

Lakini pangekuwa na nyaraka nyingine ambayo ndiyo ingekuwa imekuja rasmi mahakamani ndipo angetumia kwa usahihi Kifungu cha 75 lakini siyo kwa kumtaja shahidi aandike.

Jaji: Kwa tafsiri yangu mamlaka iliyopewa Mahakama 75(2) ni naona Mahakama inayo mamlaka kumuelekeza mtu yoyote kufanya mlinganisho wa maneno au namba kwa nia ya kuiwezesha Mahakama kufanya ulinganisho, ila huyu mtu aliye na maarifa kuliko Mahakama yenyewe.

Najiuliza kama njia yako ya kutaka shahidi asaini ni sahihi. Ka watapinga tuta shughulikia kupinga huko wakati huo

Mtobesya: Kifungu cha 47 cha Sheria ya Ushahidi ndiyo kinaruhusu maoni ya kitaalamu katika ushahidi. Lakini Kifungu cha 48 au 49, sikumbuki vizuri kinaruhusu hata mtu asiye mbobezi kufanya maoni yake

Hili Kifungu cha 75 chenyewe kinataka Mahakama kufanya ulinganisho. Leo nilikuwa na Avoid upande wa utetezi tutuzuia kutumia nyaraka hii ambayo sisi tumeipata kwenye Comito

Jaji: Na Mimi na kubaliana na wewe. Lakini kwenye document uliyonayo hatujui baada ya kumkabidhi karatasi at asaini sahihi gani kati ya hizo mbili

Mtobesya: Naomba nikabidhiwe nyaraka Original ya hati ya kuchukua mali iliyosainiwa tarehe 25 2020 inayomhusu Mohamed Ling’wenya, kwa sababu sisi tunayo moja.

Jaji: Chini ya sheria gani.

Mtobesya: Kifungu cha 246  na 146 ya Makosa ya Jinai na Sheria ya Ushahidi wa Kifungu cha 75, vyote vinafanya washitakiwa Kupewa Nyaraka zinazokusudiwa Kutumika dhidi yao kwenye makosa makubwa kama haya kupitia Comito. Kwa hiyo watupatie

Jaji: Jamani melewa

Wakili wa Serikali: Sisi haja yetu ni swala la Procedure. Ni kweli tulianika ushahidi tutaokuja kutumia mahakamani lakini ieleweka kuwa ushahidi huu ni wa kwetu. Hakuna mahala popote ambapo mteja wake anaweza kuwa na haki ya kutumia nyaraka hizo.

Angetoa basi maombi rasmi lakini hata kama ni original haiwezi kuitumia kwa  wakati huu. Haki yake ya kuhoji aendelee nayo na anaweza kuitumia hata sasa. Sisi tuna tatizo na Procedure jinsi gani ushahidi huu unataka kuletwa mahakamani

Zoezi kama hilo ni kuingiza Mahakama katika riski ambazo zinaweza kuepukika. Mheshimiwa Jaji tunatakiwa tuzingatie mfumo wetu wa utoaji haki, Mahakama kwa kutimiza wajibu wake anakuwa ni refa na siyo kwa kukaribishwa kutaka kufanya uchunguzi

Kesi ya buying wa John dhidi ya Jamuhuri criminal appeal namba 450 ya Mwaka 2017, Mahakama iliyoketi Shinyanga Katika ukurusa wa 11 paragraph ya mwisho ya ukurasa huo wa 11, ambapo swala lililojitokeza tangu wakati wa Trial Court na kesi ilikuwa ni ya ubakaji.

Ubishi ulikuwa kama mshitakiwa alikuwa ametahiriwa au haja tahiriwa. Mahakama ya Rufani ikasema kuwa hilo ni kubwa sana kwake na isingeweza kujiingiza katika risk.

Kwa kesi hii basi kama anataka Mahakama ijiridhishe. Swala ni kama nyaraka hiyo imepokelewa na kama imekubali imeandikwa na mtu huyu. Na pia kama nyaraka hiyo nyingine kama ingekuwa hapa angekuwa na haki.

Sisi tunaona ni kukiuka Procedure na a maombi hayo tunaomba uyakate mheshimiwa jaji. Na sijui ni wakati gani tena sisi tutapata kuwa na wasaa wa kuwa na shahidi huyu.

Na hilo Ndiyo dhumuni la Comito Trial kwamba mshitakiwa ajue anachokuja kujitetea nacho

Wakili Nashon Nkungu: Naona nisaidie Mahakama kama Afisa wa Mahakama, alichosema Wakili Robert Kidando amejieleza kwenye Kifungu cha 76 tu asemi kwa nini kuna haki ya kukabidhiwa nyaraka za Comito.

Na kingine Kifungu 30 cha sheria inasema tupewe copy siyo Photocopy na hapa swala la copy kwa washitakiwa halijazungumziwa wakati ni haki kwa mshitakiwa kupatiwa hiyo nyaraka

Mtobesya: Naam Mheshimiwa Jaji

Jaji: Hoja zako ulizijenga katika mazingira matatu

  1. Haki za Mahakama Jinai hasa katika Mahakama Kuu, mtu anasomewa na kukabidhi wa nyaraka, kwamba wewe unataarifa kwamba zipo nyaraka wanazolenga kuzitumia kama ushahidi wao,

Ambapo wewe umegundua sahihi katika nyaraka hizo na zilizopo hapa mahakamani sahihi zinatofautiana. Kwa maana hiyo ukaomba Mahakama ikupatia nakala halisi.

  1. Kwakuwa wanasema ushahidi huo watautumia basi wautumie mapema ili uweze kuutumia.

Mtobesya:  Mahakama I kisha fanya mlinganisho naurejesha miye nataka Mahakama I nukuu kama palikuwa na mlinganisho na kwamba Mahakama iamue kwa kuzingatia mlinganisho huo.

Jaji: nafikiri Niwape nafasi ili niweze Kurekodi mnachozungumza ili niweze kutoa maamuzi

Mtobesya: Mheshimiwa nilikuwa naomba mashauriano na Mahakama ilitusiipe Mahakama mzigo wa a kuandika Rulling

Jaji: Mnasemaje Jamhuri

Wakili wa Serikali: Ni Sawa Mheshimiwa

Jaji: Basi tuta- break kwa dakika 10, tukutane pande zote pale ofisini

Endelea kutufuatilia MwanaHALISI TV, MwananHALISI Online na mitandao yetu kujua kitakachoendelea

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!