Friday , 10 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yang’ara maonesho ya OSHA, yaibuka benki kinara yenye sera bora ya usalama, afya mahali pa kazi
Habari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho ya OSHA, yaibuka benki kinara yenye sera bora ya usalama, afya mahali pa kazi

Spread the love

KATIKA maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi duniani yanayoratibiwa kitaifa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa kazi (OSHA), Benki ya NMB imetangazwa kuwa benki yenye sera bora ya usalama na afya mahali pa kazi katika sekta ya kibenki. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akimkabithi Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi, Caroline Baraza moja ya tuzo kati ya tatu walizopokea Benki ya NMB.

Benki ya NMB katika kilele cha maonesho hayo yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro, ilinyakua tuzo tatu na kuendelea kuwa benki bora katika sekta ya fedha.

Katika kilele cha maadhimisho hayo yaliyofanyika Aprili 28 mwaka huu, NMB ilinyakua tuzo zifuatazo; Mshindi wa jumla wa kwanza katika sekta ya fedha, Sera bora ya afya na usalama mahali pa kazi kwa sekta za fedha, Banda bora katika sekta ya fedha.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya mwaka huu ambayo yamefanyika kwa mara ya 19 nchini Tanzania ni, “Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.”

Aidha, awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonesho hayo aliwataka waajiri wote nchini kuchukua hatua ya kuhakikisha wanalinda usalama na afya za wafanyakazi wao kama yalivyomatakwa ya Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi Namba 5 ya mwaka 2003.

Pia aliwaagiza kushirikiana na Wakala wa Afya na Usalama mahali pa kazi (OSHA) kuwapatia wafanyakazi elimu ya namna ya kutumia mifumo itakayostawisha mazingira ya afya na usalama mahali pa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!