WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei 1, 2023 kitaifa Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro…(endelea).
Ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 30, 2023 alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo yanahitaji maboresho.
Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Fatuma Mwasa amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tumaini Nyamhokya amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na wanamatarajio kuwa mahudhurio yatakuwa makubwa na sherehe hizo kuwa za mafanikio.
Leave a comment