Friday , 10 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Mwanga wazindua tawi jipya Arusha
Habari Mchanganyiko

Benki ya Mwanga wazindua tawi jipya Arusha

Spread the love

BENKI ya Mwanga Hakika (MHB) imezindua tawi jipya na la kisasa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutanua mtandao wake wa huduma za kifedha nchi nzima. Anaripoti Mwandishi  Wetu …(endelea).

Tawi hilo jipya lililopo katika jenga la Central Plaza, barabara ya Sokoine jirani na Clock tower jijini Arusha, linafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia saba. Matawi mengine yapo Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Mwanga na Same.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank, Eng. Ridhiwan Mringo  (wa pili kushoto) wakifungua Kitambaa cha jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha,Wanaoshuhudia pembeni ni kutoka kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na  Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo jana tarehe 29 Aprili 2023, Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo, Jagjit Singh alisema tawi hilo litaweza kurahisisha huduma kwa wateja wake na wakazi wa Arusha kwa ujumla.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha,Wanaoshuhudia pembeni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank Eng. Ridhiwan Mringo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na  Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

“Tawi hili la hapa Arusha litarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kuwa lipo kati kati ya jiji. Tawi ni la kisasa na lina sehemu maalum kwa ajili ya wateja wakubwa, vifaa vya kisasa, huduma ya kubadilisha fedha nakadhalika. Hii yote ni kuhakikisha kuwa  wateja wetu wanapata huduma bora za kisasa na kwa urahisi,” alisema.

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Benki ya Mwanga Hakika wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa tawi hilo limefunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa fursa za kiuchumi zilizopo jijini Arusha zinaweza kuwafaidisha wakazi wa jiji hilo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank Eng. Ridhiwan Mringo akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya Jijini Arusha.

 “Tawi linalozinduliwa leo (jana) ni sehemu ya mkakati wetu wa kujitanua na kuwafikia wateja wengi zaidi. Lengo letu ni kuwafikia wateja popote pale walipo lakini pia tukizingatia utoaji wa huduma bora za kifedha zinazoendana na mahitaji yao,” alifafanua.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba aliipongeza benki hiyo kwa kujikita katika kutoa huduma kwenye miradi ya miundo mbinu na kufanya kazi na  wajasiriamali wadogo na wakati.

“Napenda kuipongeza benki ya Mwanga Hakika kwa jitihada zake za kujitanua na hivyo kutoa fursa za wananchi wa kada mbali mbali kufikiwa na huduma za kifedha pamoja na kusaidia swekta mbali mbali ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!