Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Biteko: Rais Samia amewaunganisha Watanzania
Habari za Siasa

Dk. Biteko: Rais Samia amewaunganisha Watanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amewaunganisha watanzania katika sekta zote nchini ili kuhakikisha wananufaika na rasilimali mbalimbali zilizopo pamoja na kujenga uchumi wa Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kutoka Jumuiya ya Wazazi katika Maadhimisho Wiki ya Wazazi Kimkoa (Miaka 68 ya Jumuiya) yaliyofanyika leo tarehe 29 Aprili 2023 wilaya ya Chemba kwa Mtoro, Mkoani Dodoma.

“Rais Samia na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi amefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha watanzania, leo wote tunaimba maendeleo, wote tunaimba maji, wote tunaimba barabara, wote tunaimba madarasa kwa ajili ya watoto wetu na wote tunaimba maendeleo kwa ajili ya nchi yetu,” amesema Dkt. Biteko.

Akizungumzia kuhusu shule ya Sekondari Kuryo iliyosimana kwa muda mrefu amesisitiza kuwa atasimamia ili uvumbuzi upatikane na hatimaye shule hiyo ianze kufundisha.

Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko

Pia, amewataka wananchi wa wilaya ya Chemba kuungana kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo.

Katika hatua nyingine, Dk. Biteko ameitaka Jumuiya ya Wazazi wa wilaya ya chemba na Taifa kuwekeza kwa wototo ili Taifa liweze kufanikiwa kwa kuwapatia elimu na kuwafundisha malezi yaliyo bora na kuwa kizazi chenye maadili.

Naye, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa, Samwel Malecela amemshukuru Dk. Doto Biteko kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi maadhimisho hayo. Amesisitiza wananchi kupendana na kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu taratibu za nchi zilizowekwa.

Dk. Biteko ametembelea eneo la Shule ya Sekondari Kuryo na kufungua Shina la wakereketwa.
Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni “Taifa Bora, hutokana na Malezi Bora ya Watoto”. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa, Mbunge wa Jimbo la Chemba Mohamed Monni na wananchi wa wilaya hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!