BENKI ya NMB imetoa udhamini wa Sh. milioni 25 kwa Mashindano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi Tanzania (NMB CDF Trophy 2022), kama muendelezo wa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambayo hufanyika Septemba mosi.
Sherehe za kumbukumbu hizo kwa mwaka huu yamelazimika kusogezwa kwa mwezi mmoja kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akizungumza wakati akipokea mfano wa hundi Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwa mdhamini wa muda mrefu na kufanyia maboresho zaidi kwa mwaka huu.
Alisema timu mbalimbali zimethibitisha kushiriki michuano hiyo, ambayo itahusisha makundi ya Watoto (junior), Madaraja (division) ya A, B, na C, pamoja na wanawake na Seniors.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum wa Benki ya NMB, Getrude Mallya, alisema benki yake imedhamini mashindano hayo kwa Sh. milioni 25.
Pia aliwaalika viongozi wa klabu ya gofu Lugalo kushiriki mbio za NMB Marathon 2022 ‘Mwendo wa Upendo’ zitakazofanyika Oktoba 1, 2022 katika viwanja vya Leaders Club kwa lengo la kukusanya Sh. milioni 600 za kusaidia matibabu ya kina mama wenye matatizo ya fistula nchini.
Mashindano ya Gofu yatafanyika Oktoba 1 hadi 2 mwaka huu kwenye Viwanja vya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.
Leave a comment