October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwigulu:Mashauri ya kodi ya Trilioni 360/- yalifutwa

Dk. Mwigulu

Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema mashauri ya kikodi ya Sh 360 trilioni yalifutwa kufuatia makubaliano ya Serikali na kampuni ya madini ya Barrick Corporation mwaka 2020. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mwigulu ameyasema hayo leo Ijumaa tarehe 23, 2022, akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina aliyetaka kujua kwanini mashauri ya kikodi 1097 yenye thamani ya Sh 360 trilioni na dola milioni 181.4 hayajafanyiwa uamuzi.

Swali hillo liliulizwa jana lakini halikuapiwa majibu ya kuridhisgha na hivyo Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson kumwagiza Dk. Mwigulu kulijibu kwa usahihi kama ambavyo liliulizwa.

Mwigulu amesema Serikali haina mashhauri hayo na badala yake mashauri yaliyopo hadi kufikia Agosti 2022, ni 854 yenye thamani ya Sh. 4.2 na dola za Marekani milioni 3.4.

Akiuliza swali la nyongeza Mpina alisema mashauri hayo yametajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2019/2020 na kutaka kujua kwanini Serikali ilifuta mashauri hayo na kukubali kupokea Sh 700 bilioni.

Akijibu swali hilo la nyongeza Dk. Mwigulu alifafanua kuwa ni kweli kwamba mashauri hayo yalikuwepo kwenye ripoti ya CAG na kwamba yaliibuka mwaka 2028 baada ya Serikali chini ya Rais wa amwamu ya nne Hayati Dk. John Magufuli kuunda timu ya uchunguzi iliyokuja na madai hayo.

Amesema hata hivyo mashauri hayo yalifutwa baada ya makubaliano ya Serikali na kampuni ya Barrick ikiwemo kuundwa kwa kampuni ya ubia ambyo Serikali itamiliki asilimia 16 pamoja na mgawanyo wa faida za kuichumi asilimia 50 kwa 50.

Alisema makubaliano mengine ilikuwa ni Barrick kufuta kesi ya dola 2.7 bilioni dhidi ya Serikali,  kuilipa Serikali Dola milioni 300, kutoa dola milioni 40 za ukarabati wa barabara na kutoa dola sita katika kila wakia ya dhahabu na dola milioni 10 za ujenzi wa maabara ya madini.

“Makubaliano haya yaliisha tarehe 24 Januari mwaka 2020 na sherehe hizi zilifanyika Ikulu mbele ya Rais Magufuli na Tanzania tukakubali kuachia Sh 360 trilioni tumalize shauri lile na tukaunda kampuni ya Twiga na nchi nzima tulisherehekea kuwa na asilimia 16 ya kampuni,” amesema Mwigulu.

Amesema baada ya makubaliano hayo kilichofanyika ni kuanza kupokea gawio ambapo 2021 na mwaka 2022 walipokea gawio ya kile kilichokubaliwa.

error: Content is protected !!