Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaalika wachimbaji wadogo, kati kuchangamkia mikopo ya mitambo
Habari Mchanganyiko

NMB yaalika wachimbaji wadogo, kati kuchangamkia mikopo ya mitambo

Spread the love

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwainua wachimbaji wadogo na wa kati kwenye sekta ya madini, Benki ya NMB imetoa wito kwa wachimbaji hao kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo itakayowawezesha kununua mitambo itakayorahisisha shughuli hiyo ya uchimbaji.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 29 Septemba, 2022 na Afisa Uhusiano wa benki hiyo mkoani Geita, Mussa Nyango wakati akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo kuhusu ushiriki wa NMB katika maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

 

Afisa Uhusiano wa benki ya NMB mkoani Geita, Mussa Nyango (kushoto) wakati akimuelezea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo (kulia) kuhusu ushiriki wa NMB katika maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Nyango amesema katika banda la benki hiyo lililopo katika viwanja hivyo, huduma zote za kibenki zinapatikana ikiwamo kufungua akaunti, huduma ya kuweka na kutoa pesa kwa njia ya wakala na huduma nyingine.

Akizungumzia kuhusu mikopo kwa wachimbaji wadogo, amesema NMB ilijipanga na inaendelea kutoa mikopo kwa wachimbaji hao wadogo, wa kati na wakubwa kwa lengo la kuimarisha shughuli za uchimbaji nchini.

Amesema mikopo hiyo imewawezesha baadhi ya wachimbaji wadogo kukua na kuingia katika kundi la kati kutokana na mitambo ya kisasa waliyoinunua katika shughuli za uchimbaji.

Mbali na wachimbaji hao, amesema benki hiyo inatoa wito pia kwa wajasiriamali wadogo kujiunga na NMB ili kupata mikopo itakayowawezesha kukua kibiashara.

Aidha, akizungumzia jitihada hizo za NMB, Naibu Waziri huyo mbali na kuipongeza benki hiyo, pia alitoa wito kwa wachimbaji wadogo kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kupata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali yanayohusiana na kukuza sekta ya madini nchini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo akisaini kitabu cha wageni katika banda la NMB

Maonyesho hayo yanayofanyika kila mwaka, kwa mwaka huu yameshirikisha washiriki zaidi ya 600 wakiwemo 12 kutoka nchi mbalimbali ambao wanaonyesha teknolojia ya uchimbaji wa madini.

Maonyesho hayo ya tano ya kitaifa ya teknolojia ya madini kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya “Madini na fursa za uchumi ajira kwa maendeleo endelevu”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!