Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB mlipa kodi mkubwa na bora zaidi Tanzania 2023
BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB mlipa kodi mkubwa na bora zaidi Tanzania 2023

Spread the love

Benki ya NMB imeibuka mshindi wa jumla kitaifa katila kundi la mlipa kodi mkubwazZaidi Tanzania lakini pia katika kundi la mlipa kodi bora zaidi anayelipa kodi kwa hiari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

NMB imenyakua tuzo hizo jana Ijumaa katika hafla ya walipa kodi wakubwa kwa 2022/2023 iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Ushindi huo unaifanya NMB kubeba tuzo hizo zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mwaka wa pili mfululizo

Jumla ya tuzo ilizopata NMB ni: Mshindi wa jumla kitaifa: Taasisi inayolipa Kodi kubwa zaidi nchini Tanzania (Sekta zote).

Pili, Mshindi wa jumla kitaifa: Taasisi bora inayolipa kodi kwa hiari kwa  kuzingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (Most Compliant Tax Payer).

Tatu ni mshindi wa kwanza: Mlipa kodi mkubwa zaidi katika kundi la taasisi za fedha nchini Tanzania (mara ya tatu mfululizo).

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema tuzo hizo ni matokeo chanya ya misingi imara ya utawala bora na uadilifu, kuzingatia kanuni za ulipaji kodi, ufanisi katika kuendesha biashara na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha kwa wateja.

Ruth Zaipuna aliwashukuru wateja wa NMB na Watanzania wote kwa kuendelea  kuiamini benki hiyo kama mshirika wao kwenye biashara na shughuli zao.

“Ninaishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini na kipekee nawashukuru wafanyakazi wenzangu wote wa NMB kwa kuendelea kufanya kazi kwa ari, bidii na kwa uzalendo mkubwa kwa maslahi mapana ya Benki na nchi yetu kwa ujumla,” alisema.

Tuzo hizo za TRA zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Kama mdau wa maendeleo, NMB tutaendelea kuendesha biashara yetu kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuendelea kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Taifa letu,” alisema Zaipuna.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Mchezo wa maokoto Cobra Queen unapatikana Meridianbet

Spread the love Meridianbet Kasino Mtandaoni utapata fursa ya kufurahiamchezo uliochochewa na...

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Biashara

Pata Mil 450 ya Non Stop Drop ukicheza Meridianbet kasino

Spread the love  JIUNGE na promosheni ya Kusisimua iitwayo NON-STOP DROP, inayotolewa...

Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love  BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s...

error: Content is protected !!