Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB kukopesha hadi bilioni 250 mtu mmoja
Habari Mchanganyiko

NMB kukopesha hadi bilioni 250 mtu mmoja

Spread the love

UFANISI mkubwa wa kiutendaji ambao Benki ya NMB imeupata miaka ya hivi karibuni umeiwezesha taasisi hiyo kinara wa huduma za kifedha nchini kuimarika kiufadhili. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Viongozi wake waandamizi wamebainaisha mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa miongoni mwa matokeo ya kufanikiwa huko kifedha ni kuiwezesha benki hiyo kuongeza kiasi cha mkupuo mmoja wa mkopo kwenye miaka ya hivi karibuni

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Mtandao wa Wateja Wakubwa na Wanaochipukia (BEN) wa NMB, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa benki hiyo, Benedicto Baragomwa, alisema kiwango kikubwa cha mkupuo mmoja wa mkopo sasa kimefikia Sh 250 bilioni.

Mkuu wa wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija (wapili kushoto) akisalimiana na Mkaguzi mkuu wa Ndani wa benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wapili kulia) katika hafla ya kukutana na wateja wakubwa wa Benki ya NMB katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mstahiki Meya wa jiji la Ilala, Omar Kumbilamoto na kulia ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard.

Kiasi hicho ni kikomo cha kikanuni ambacho benki hiyo inaweza kumkopesha mteja mmoja kwa mkupuo.

Hilo limewavutia sana wateja wa NMB na viongozi wa jiji na mkoa wa Dar es Salaam walioudhuria mkutano huo walioipongeza kwa hatua hiyo kubwa kiufadhili na kusema ni matokea ya uwezo wake kiubunifu na uwekezaji wa kizalendo inaoufanya nchini.

“Sisi ndio mkopeshaji mkubwa mwenye viwango vya faida ambavyo havina mpizani sokoni na haina tofauti tofauti za huduma za mikopo kama ile ya dharura inayopatikana papo kwa papo kidijitali kwa kutumia simu za mkononi,” Baragomwa aliwaambia washiriki 100 wa mkutano wa BEN wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya namna hii iliyofanyika pia katika jiji la Mbeya, mkuu wa idara ya mikopo wa benki ya NMB, Demetus Kamguna alisema sasa hivi NMB inajivunia kuwa na mizania mipana yenye rasilimali zenye thamani ya takribani TZS trilioni 9 pamoja na amana zipatazo TZS trilioni 6.6.

Aidha, alisema kukua kwa mali zake zote kumesaidia kupanua kiasi cha mtaji wake hadi zaidi ya TZS trilioni 1 na kupelekea kuzidisha ukomo wa mkupuo mmoja kwa kila mkopaji mwenye sifa.

“Pia NMB tunatoa mikopo kadri ya uwezo wa mfanyabiashara, tukiwa na uwezo wa kutoa hado TZS bilioni 250 kwa mkopaji mmoja,” kiongozi huyo mwandamizi alisema kwenye mchapalo huo wa kujadili masuala muhimu na wateja wake wakubwa wa Mkoani Mbeya uliofunguliwa rasmi ya Mkuu wa Mkoa ya Mbeya,” amesema Juma Homera.

Akielezea kiwango kipya cha mkupuo wa juu wa mkopo kwa kila mteja, Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Alex Mgeni, alimwambia waandishi wa habari kuwa maendeleo ya ukopeshaji yaliyopatikana pia ni matokea chanya ya faida kubwa ambazo NMB imekuwa ikipata miaka ya hivi karibuni.

Pamoja na mambo mengine mengi, faida za NMB zimekuwa pia zikitumika kuimarisha utendaji na uendeshaji wa benki hiyo na pia kudhatiti mtaji wake. Matokeo ya uwekezaji huo, Bw Mgeni alifafanua, ni pamoja na kuongeza kiwango cha NMB kuwakopesha wateja wake.

“Kimsingi, mtaji wetu sasa ni TZS trilioni 1.2 ambazo zinapelekea mkupuo mmoja wa mikopo yetu kufikia hadi TZS bilioni 300 kwa kuzingatia kanuni ya Benki Kuu ya benki kukopesha asilimia 25 ya mtaji wake,” alisema Mgeni

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkuu wa mkoa wa Mbeya aliwasihi Benki ya NMB kuendelea kuwaunga mmono wakulima kwani ni sekta inayokuwa kwa kasi sasna kwa hivi Karibuni huku akisisiktiza juu ya kuendelea kuwek nguvu kubwa katika ufadhili wa kilimo cha maparachichi, mchele na pareto.

Aidha, katika hafla ya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw Ludigija, aliimwagia sifa NMB kwa kuja na wazo la BEN akisema si muhimu tu kwa ajili ya kupata mrejesho kutoka kwa wateja lakini pia kusaidia kuchangia mawazo ya sera za kitaifa.

NMB ilianzisha mtandao wa BEN mwaka 2014 ikilenga kuitumia mikutano yake kama jukwaa la kukutana na wateja wake wenye mzunguko wa fedha kuanzia TZS bilioni 5 kwa mwaka kwa ajili ya kubadirishana wazo na uzoefu wa kibiashara.

Mpango huo ulilenga mikoa mikubwa na inayoongoza kiuzalishaji na mpaka sasa, mtandao huu upo kwenye mikoa saba tu ambako ina washirika zaidi ya 1,000. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Arusha na Mbeya.

Kwa upande wake, Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto, alisema NMB sasa ni mshirika wa kimkati wa maendeleo ya kibiashara wa kitaifa ambaye anaisaidia Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!