Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia, Ruto wakubaliana mambo 7, biashara yazidi kupaa
Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Samia, Ruto wakubaliana mambo 7, biashara yazidi kupaa

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema wamekubaliana mambo saba kati yake na Rais wa Kenya, Dk. William Ruto na kusisitiza kuwa ziara kiongozi wa taifa hilo la Kenya nchini ni fursa adhimu na muhimu kwao.

Amesema ziara Ruto ya siku mbili nchini inawawezesha kukaa pamoja kama majirani na ndugu wa damu kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa maendeleo na ustawi wa mataifa hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Oktoba, 2022 wakati viongozi hao wakizungumza na waandishi kuhusu mambo waliyokubaliana katika mazungumzo yao.

Amesema wamejadiliana masuala mengi ya mkakati wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye ukanda na kimataifa.

“Mosi; Tumekubaliana kukuza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, kama mnavyoelewa Tanzania na Kenya ukiacha mipaka ya kiutawala, mambo mengine tuko wamoja, tuna mpaka mkubwa ambao watu wetu wanashirikiana na biashara zinakwenda mambo yetu ni mamoja,” amesema.

Pia Rais Samia amesema wamekubaliana kuimairisha ushirikiano wa kibiashara ambao hapo awali ulianza kufanyiwa kazi na Rais Uhuru Kenyatta kwa kuwataka wataalam wa nchi hizo mbili kufanyia kazi vikwanzo vya kibiashara vilivyopo.

“Kwa ujumla walitambua vikwazo 68 ambavyo vilifanyiwa kazi na 54 visivyo vya kikodi viliondolewa, vimebaki vikwazo 14, tumetaka mawaziri wetu wa sekta ya biashara na uwekezaji wakutane haraka kufanyia kazi.

“Kwa ujumla kazi iliyoanza baina yetu Tanzania na Kenya, imekuza sana biashara, Ruto alitoa takwimu akasema Tanzania mmefaidika mara mbili zaidi ya vile mlivyokuwa mmefaidika. Lakini ikifaidika Tanzania imefaidika Kenya pia, kwa sababu Kenya na Tanzania tusigawane umaskini na udhalili, lakini tugawane utajiri utakaotokana na biashara,” amesema.

Tatu; amesema wamekubaliana kuwaagiza mawaziri wa mambo ya nje wa pande zote mbili, Dk. Stargomena Tax (Tanzania) na Alfred Mutua (Kenya) wakutane haraka wazungumze mambo yanayohusu ajenda ambazo zipi kweny mkutano wa nne wa tume ya ushirikiano ambao ulitakiwa kufanyika Agosti, 2022.

Suala la nne ambalo wamekubaliana viongozi hao ni kuimarisha zoezi mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili.

“Ni vema kwa sababu tunarithisha watoto wetu ambao wanatakiwa kujua mipaka imepita wapi ingawa kiutamaduni, ki-damu hatuna mipaka lakini tuna mipaka ya kiutawala. Kazi hii ilishafanywa vizuri na sasa watalaam wetu wakakae waangalie uwezekano wa kuendesha zoezi hili awamu ya pili, amesema.

“Tano; Kuna mradi wa bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Dar es salaam kwenda Mombasa ambao tulishasaini makubaliano pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, lakini Rais Ruto ameubeba kuwa mradi wake wa kwanza atakaoanza na Tanzania.

“Sita; Tumezungumzia pia kushirikiana kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyovuka mpaka na hapa tumvitaka vyombo  vyetu vya ulinzi na usalama, kushirikiana kwa karibu na kuangalia makosa yanayovuka mpaka.

“Makosa kama vile dawa za kulevya, uharamia, ujangili, masuala ya kusafirisha watu, tumetaka wakae waangalie kwa nchi zetu mbili tutafanya vipi kudhibiti vitendo hivi kwa sababu tumepata sifa mbaya wakati wanaosafirisha sio watanzania, sisi tunakamata tu, lakini rekodi za zinaiona Tanzania,” amesema.

 Mwisho amesema wakubaliana kushirikiana katika masuala ya kikanda na kimataifa.

“Tumekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri na madhubuti kwenye Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa  lakini hasa ndani ya Afrika Mashariki kwamba Kenya, Tanzania na Uganda ndio viongozi wakuu wa EAC, kwa hiyo hatuna budi kushirikiana ili wanaoungana nasi wakute kuna ushirikiano madhubuti uliojengwa nasi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!