Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ni uvamizi, unyanyasaji na mauaji tu Palestina
Kimataifa

Ni uvamizi, unyanyasaji na mauaji tu Palestina

Spread the love

WAKAZI wa Palestina ni moja ya raia wanaoishi katika mateso makubwa ndani ya ardhi yao. Wananyanyaswa, wanateswa na hata kuuawa. Kutoka katika mitandao ya kimataifa….(endelea).

Haya ndio maisha yao kwa miaka mingi iliyopita. Kinachowatesa mpaka sasa ni wema uliofanywa na mababu zao. Ardhi yao inaendelea kupokwa na Israel licha ya wito wa kutakiwa kuacha kufanya hivyo.

 Mpaka sasa Israel inaendelea kujitanua kwa kuvamia maeneo yao. Hatua zake hizo zinakinzana na mikataba mbalimbali ambayo iliwahi kuiingia.

 Uvamizi wa hivi karibuni ulifanywa Jumatatu asubuhi ya tarehe 22 Julai 2019). Israel iliamua kuvamia eneo la Sur Buher liliopo Jeruslem ya Mashariki.

 Ilibomoa majengo 10 yaliyoko karibu na ukuta uliojengwa na Israeli kwenye ardhi ya Palestina. Uvamizi huo umesababisha kuathiri maisha ya Wapalestina 300.

 Hatua hiyo, ni mwendelezo wa kuvunja makubaliano ya amani ya ya kimataifa ya Oslo (Oslo accords), kati ya Palestina na Israel kuhusu utawala wa maeneo mbalimbali.

 Kwa mujibu wa mkataba huo na maazimio ya Umoja wa Mataifa (UN), eneo la Sur Buher ambalo lipo ndani ya “Area A,” liko chini ya mamlaka na uongozi wa Palestina.

Mkataba wa Oslo ni makubaliano yaliyosainiwa kati ya Serikali ya Israel na Shirika la Ukombozi la Palestina (PLO) mwaka 1993, lengo likiwa kumaliza mgogoro na kuleta amani.

Katika makubaliano hayo, Israel na Palestina ziliridhia mgawanyiko wa maeneo mbalimbali huku wakikubaliana kuwa “area A” ni sehemu ya Palestina.

 Lakini mwaka 2002, Israel ilikiuka mkataba huo na kujenga ukuta kwenye eneo hilo (Area A) kwa madai ya kujihakikishia ulizi na usalama.

 Mwaka 2004mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), ilijitokeza waziwazi na kulaani hatua ya Israel kuvamia eneo hilo na kuweka makazi.

 Uvamizi huo umelalamikiwa na Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, akieleza kuwa unyanyasaji na uharibifu katika ardhi ya Palestina unaofanywa na Israel unapuuza sheria za kimataifa.

 Hata hivyo, Rais Abbas ameelekeza tuhuma zake ni sehemu ya mpango wa kutekeleza “Deal of Century” (mpango wa amani wa Donald Trump) ambao unakusudia kutupilia mbali swala na haki za Wapalestina.

 Rais Abbas ameitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati mara moja kumaliza uhasama huu dhidi ya Wapalestina. Umoja wa Nchi za Kiarabu umelaani uharibifu huo uliofanywa na Israeli katika eneo la Sur Baher.

 Saeed Abu Ali, Katibu Msaidizi wa Umoja wa Nchi za Kiarabu anayehusika na maswala ya Palestina, amesisitiza kwamba kinachotokea Sur Buher, ni uhalifu wa kivita na utakaso wa kikabila.

 Amesema, majengo yanayobomolewa yako kwenye eneo A (Area “A”) chini ya mamlaka ya Palestina.

 Ufaransa kwenye taarifa yake imeeleza, ubomoaji wa maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya Palestina yanapingana na sheria za kimataifa, hususani sheria za kimataifa za kibinadamu na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

 Sufian Qudah, Msemaji Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi ya Jordani amesisitiza, Jordani inapinga sera za makazi ya Israeli, pamoja na ujenzi na upanuzi wa makazi katika maeneo yanayotawaliwa na uongozi wa Palestina.

 Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC), limeishurumu Israel kwa uharibifu huo katika makazi ya Wapalestina likisisitiza kwamba, ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kibinadamu za kimataifa.

 Katika taarifa yake, NRC imesema, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Israeli imebomoa majengo 140 yanayomilikiwa na Wapalestina katika mji huo (kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu OCHA).

 Jamie McGoldrick, Mratibu wa Huduma za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa; Gwyn Lewis, Mkurugenzi wa Operesheni za Mji wa West Bank kwa pande wa UNRWA na James Heenan, Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Palestina, wameeleza kuhuzunishwa na hatua ya Israel kuvamia na kukwapua sehemu ya ardhi ya Sur Buher.

 Jumuiya ya Ulaya pia imetangaza katika taarifa kwamba, uhamishaji na uharibifu wa Israel ni haramu chini ya sheria za kimataifa, na kutoa wito kwa taifa hilo kuacha mara moja uharibifu huo.

 Ni kutokana na majengo hayo kuwa katika eneo A la Mji wa West Bank ambapo kulingana na makukubaliano ya Oslo, maswala yote ya kiraia na ujenzi katika eneo hilo yapo chini ya mamlaka ya Palestina.

 Nchi zingine ikiwa Algeria, Urusi, Uturuki, Ujerumani, Uhispania na Ubelgiji zimetoa tamko kuikemea Israeli kwa uvamizi huo.

 Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imesema, itaongeza juhudi katika kuhakikisha kwamba Israel inawajibika kwa makosa hayo ya kivita dhidi ya wakazi wa Sur Buher.

Katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliyofanyika Jumanne 23 Julai 2019, nchi mbalimbali zilitoa malalamiko yake dhidi yaunyama wa Istael kwa Wapalestina. Nchi hizo ni;-

 Afrika Kusini, Senegal, Moroko, Côte d’Ivoire, Namibia, Uganda, Egypt, Guinea ya Ikweta, Kuwait , Ujerumani, Poland, Uchina, Ubelgiji, Uingereza, Jamhuri ya Dominika, Ufaransa, Indonesia, Peru, Japan, Brazil, Argentina, Pakistan na Jordan.

 Pia zimo Chile, Qatar, Malaysia, Uruguay, Ecuador, Bangladesh, Uturuki, Norway, Cuba, Maldives, Venezuela, Bahrain na Falme za Kiarabu.

 Mataifa mbalimbali yameonesha kukerwa na uporaji na manyanyaso yanayofanywa na Israel dhidi ya Palestina lakini jambo la kujiuliza, ni kitu kani kinaweza kuiokoa Palestina kutokana na mateso hayo ya Israel?

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Ayatollah Khamenei aongoza wairan kumuaga Raisi

Spread the loveKiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Kimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!