May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ni maafa Indonesia, 76 wafariki dunia

Spread the love

 

JUMLA ya watu 76 wamefariki dunia baada ya kuvamiwa na tope la volcano, mafuriko na upepo mkali nchini Indonesia. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Mkasa huo umetokea jana Jumapili tarehe 4 Machi 2021, ambapo taarifa zaidi zinaeleza, kimbunga kilichopewa jina la Cyclone Seroja kimeathiri zaidi maeneo mbalimbali ya taifa hilo.

Katika Mji wa Nusa, taarifa zinaeleza jumla ya watu 55 wamefariki dunia huku 55 hawajulikani walipo, ni baada ya Kimbunga cha Seroja cyclone kupiga mji huo na kusababisha mafuriko, maporomoko ya udongo na upepo mkali.

Taarifa zinaeleza, jumla ya watu 400 wameondolewa eneo hilo kutokana na kuwepo kwa upepo mkali, pia mvua kubwa inaotishia usalama wa eneo hilo.

Eneo lingine lililoathirika kutokana na upepo huo ni pamoja na Kusini mwa Mji wa Nusa Tenggaraambapo mamia ya watu wameondolewa eneo hilo.

Katika Mji wa Timor, inaripotiwa watu 21 wamefariki dunia kutokana na volcano ya tope, mafuriko na kuangukiwa na miti kutokana na upepo mkali.

Katika maeneo mbalimbali nchini humo inaelezwa, zaidi ya watu 1500 wameondolewa kwenye maeneo yao kupisha upepo mkali unaoanzia Bahari ya Savu na kutishia amani katika maisha yao.

Mkurugenzi wa Ulinzi wa Jamii nchini humo, Ismael da Costa Babo amesema, madaraja pamoja na miti vimeanguka na kusababisha baadhi ya barabara kutopitika.

“Madaraja na miti mingi imeanguka kutokana na upepo mkali, hivyo kuna baadhi ya barabara haziwezi kupitika kwa sasa.”

“Pia, madhara yametokea baharini ambapo kuna meli moja imeshindwa kuendelea na safari kutokana na upepo mkali,” amesema.

Katika Kisiwa cha Lembata, imeripotiwa watu 20 wamefariki dunia, na kwamba baadhi ya maiti zimeonekana zikieleza baharini.

“Tunatumia boti kutafuta miili mingine baharini. Vijiji vingi Lembata vimeathiriwa kutokana na mkasa huo kutokea usiku watu wakiwa wamelala,” Thomas Ola Langoday, Mkuu Msaidi wa Wilaya ya Lembata kisiwani humo.

Rais wa Indonesia, Joko Widodo ametuma salama za pole kwa watu waliofikwa na mkasa huo, akisisitiza wananchi kufuata maelezo wanayopewa ili kuepuka maafa zaidi.

error: Content is protected !!