May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua, atumbua bosi TPDC

Thobias Mwesiga Richard

Spread the love

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Mwesiga Richard. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Richard aliteuliwa jana usiku Jumapili, tarehe 4 Aprili 2021, kushika nafasi hiyo.

Ikiwa ni saa chache zimepita tangu kuteuliuwa, leo Jumatatu asubuhi, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema, Rais Samia ametengua uteuzi huo na kumrejesha Dk. James Mataragio.

Dk. Mataragio, amerejeshwa kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC.

Dk. Mataragio ndiye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC kabla ya uteuzi Richard kutangazwa jana Jumapili na ametakiwa kuendelea na majukumu yake mara moja.

error: Content is protected !!