Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NGO’s zatoa vilio vya kodi, TRA yaziita mezani
Habari Mchanganyiko

NGO’s zatoa vilio vya kodi, TRA yaziita mezani

Meneja wa TRA Kinondoni, Edmund Kawamala,
Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetakiwa kutatua changamoto za kodi zinazokabili Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), zisizoingiza faida. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 30 Juni 2023, jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa nusu mwaka kati ya TRA na NGO’s, kuhusu masuala ya kodi kwa mashirika ya uhisani.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya NGO’s Tanzania, Mwantumu Mahiza, ameitaka TRA kukaa mezani na mashirika hayo kwa ajili ya kujadili changamoto zao Kisha kuzitafutia ufumbuzi.

????????????????????????????????????

Aidha, Mahiza ameitaka TRA kupanua wigo wa utoaji elimu ya ulipaji kodi nchi nzima, ili kuziwezesha NGO’s kujiendesha kwa kufuata sheria kwa ajili ya kukwepa kufungiwa kwa kuwa zinaajiri vijana wengi pamoja na kuzisaidia Jamii.

“Sio kwamba ninawatetea sana, Bali hebu fungueni macho hizi NGO’s ziko zaidi ya 8,000 tukisema tuzifute Hali itakuaje? Kuna kazi zinafanywa kwa ufanisi na NGO’s ambazo Serikali hatufiki kwa kiwango kinachokusudia,” amesema Mahiza.

Akiwasilisha changamoto za NGO’s, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amesema kumekuwa na changamoto katika sera ya mashirika yanayofanya uhisani, ambazo zinapelekea mizigo yao inayoingizwa nchini kukwama kutokana na kudaiwa kodi.

“Sera ya Charitable status (mashirika ya uhisani) ni changamoto kubwa, nadhani ni muda muafaka kuangalia sheria ya Charitable Status ili mashirika mfano yanaoeta gari kuhudumia Jamii kwa Nini lilipiwe  kodi wakati linaletwa kuhudumia jamii,” amesema Olengurumwa.

Changamoto nyingine iliyotajwa na Olengurumwa ni ya NGO’s kuanzia kutozwa kodi mara moja inaposajiliwa bila kujali kama ina fedha au lah, ambapo ameshauri zipewe muda wa huruma wa miaka mitano ili kujiimarisha kiuchumi.

“Tunashauri NGO’s zipewe grace period ya five years, hapa tunazungumzia Kodi za kitaasisi lakini kama umeajiri wafanyakazi lazima ulipe.

Tunaomba muda wa huruma sababu kuanzisha NGO’s sio suala la rahisi uweze kusimamia. Kuna makampuni yanapewa grace period miaka 10 kwa nini isiwe sisi tunaohudumia wananchi,” amesema Olengurumwa.

Pia, Olengurumwa ameshauri Kodi ya ongezeko la thamani (VAT), isitozwe kwa mashirika ya uhisani kwa kuwa hayafanyi biashara.

“Kuhusu masuala ya EFD inatupa changamoto NGO’s wanalalamika wanafanya kazi maeneo ya vijijini lakini EFD imekuwa shida baadhi ya maeneo hakuna. NGOS haitakiwi kuwa na EFD lakini unaofanya nao huduma lazima wawe na EFD sasa shida maeneo ya vijijini hawana,” amesema Olengurumwa.

Katika hatua nyingine, Olengurumwa ameshauri zitungwe kanuni maalum za kodi, kwa ajili ya mashirika yasiyoingiza faida bali zinafanya kazi za uhisani wa kuzisaidia jamii.

Akijibu changamoto hizo, Meneja wa TRA Kinondoni, Edmund Kawamala, amezitaka NGO’s zenye malimbikizo ya faini kuandika barua ili zifutwe.

“Tunafuta ili kumpa mwanga kufanya kazi sababu akiona mafaili mengi ya adhabu itamnyong’onyesha hata kulipa Kodi,” amesema Kawamala.

Aidha, Kawamala,  amezitahadharisha akisema “uamuzi wa kufuta faini haimaanishi muendelee kutowasilisha return, nitayoa elimu ya jinsi ya kutoa return ili NGO’s zisiwe zinafutwa kwa sababu hiyo. Pale kwangu hakuna appointment mje wakati wowote nitawasikiliza.”

Kuhusu Malalamiko ya VAT, Kawamala amesema NGO’s zisizofanya biashara hazitozwi kodi hiyo, bali zinazotozwa  ni zile zinazofanya biashara.

Kwa upande wa msamaha wa kodi kwa vitu vinavyoagizwa na NGO’s, Kawamala amesema sheria imeweka sharti hilo ili kuwadhibiti watu wanaoweza tumia mwanya huo vibaya kuingiza vitu kwa maslahi yao binafsi hususan kibiashara kwa ajili ya kukwepa kodi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!