Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NGOs zabisha hodi kwa Rais Samia
Habari Mchanganyiko

NGOs zabisha hodi kwa Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

MASHIRIKA Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yameomba kuonana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ili kumkabidhi changamoto zao zilizoshindwa kutatuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa katika Jukwaa la Mwaka la NGO’s kwa 2023, linalofanyika jijini Dar es Salaam, kuanzisha leo Ijumaa hadi kesho tarehe 29 Julai mwaka hii.

Miongoni mwa changamoto zinazolalamikiwa na mashirika hayo, ni kutozwa kodi kama taasisi zinazofanya biashara, kuikosa hadhi ya mashirika yanayotoa msaada na kukwama kupata namba za mlipa kodi (TIN number).

Akizungumza katika mjadala huo, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Usawa wa Kijinsia Tanzania (SUKITA), Msafiri Mwajuma Mariam, amedai changamoto wanazokutana nazo ni kutozwa kodi kubwa, kulazimishwa kuzuia Kodi ya majengo kitendo kinachozuia mgogoro baina Yao na wamiliki wa nyumba wanazopanga.

“Changamoto nyingine tukiomba misamaha ya kodi tunachelewa kupata, wako wengine wameiomba mpaka leo hawajapewa. TRA umsitulazimishe kumfikia mama wakati ninyi mnaweza. Mnatushawishi kumtafuta Rais Samia ili atutatulie shida zetu,” amesema Msafiri.

Naye Mgonja, ameshauri sheria inayosimamia NGO’s, irekebishwe  ili mashirika yanaposajiliwa yapatiwe hadhi ya kutoa misaada, badala ya utaratibu uliopo Sasa wa kusubiri miaka mitatu baada ya kaunzishwa.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa ameitaka TRA isitoze Kodi fedha ambazo NGO’s zinapokea kutokana na michango ya matembezi ya hiari, kwa kuwa ni fedha za ufadhili.

“Fedha za matembezi ya hiari huo ni mchango kama ruzuku nyingine, inaingia kwenye Shirika kama ruzuku. Pia, changamoto nyingine inavyopaswa kutatuliwa ni NGO’s kupata charitable status, inabidi itatuliwe,” amesema Olengurumwa.

Pia, Olengurumwa ameiomba Serikali itoe msamaha wa jumla kwa NGO’s, pamoja na kuondoa takwa la mashirika yasiyopata fedha za miradi, kuwasilisha taarifa za Mapato na matumizi kila mwezi.

Katika hatua nyingine, wadau hao wameitaka TRA kushirikiana na NGO’s ili wajifunze namna zinavyofanya kazi, kitendo kitakachoondoa migongano baina ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Msajili wa NGO’s, Vicky Mayao, amezitaka NGO’s kuunda kamati Maalum itakayokusanya malalamiko yao ya kikodi kwa ajili ya kufikisha TRA ili uafanyiwe kazi.

“Kuna kamati ndogo ya kikodi ilianzishea, nasema warudi mezani sababu sheria za kodi zipo hatuwezi kuzibadilisha hapa, hata tunavyomtaka kamishna hawezi kuja hapa natamani turudi kwenye kamati ya Majadiliano,” amesema Mayao.

Kufuatia malalamiko hayo, Afisa kutoka TRA aliyejitambulisha kwa jina la Mario, amesema changamoto zote zitawasilishwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!