Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML yatoa msaada wa madawati 8,823 mkoani Geita
Habari Mchanganyiko

GGML yatoa msaada wa madawati 8,823 mkoani Geita

Spread the love

KATIKA kutimiza dhamira ya kuimarisha sekta ya elimu na kuwezesha mazingira ya utoaji elimu nchini kuwa ya usawa, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa msaada wa madawati 8,823 kwa shule mbalimbali za Geita ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi wa mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika juzi Mjini Geita kwa ushirikiano na mamlaka za serikali za mitaa kupitia mpango wa GGML wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka.

Alisema kadiri shule nyingi zinavyoendelea kujengwa ndivyo hitaji la madawati linavyozidi kuonekana jambo ambalo GGML inajitahidi kutatua changamoto hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela baadhi ya viongozi wengine wa mkoa huo, wakiwa wamekaa katika madawati hayo pamoja na wanafunzi mkoa huo kama ishara ya furaha ya makabidhiano ya madawati kwa shule mbalimbali za Geita.

Shigella alipongeza GGML kwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya kuinua sekta ya elimu mkoani Geita na Tanzania nzima kwa ujumla.

“Ni furaha yangu kwamba tangu GGML ianze shughuli za uchimbaji hapa mkoani Geita, imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Serikali kutekeleza miradi kadhaa ya elimu, hasa ujenzi wa madarasa na shule”.

Mkuu huyo wa mkoa alikiri kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule mbalimbali hivyo kuwaomba wadau wengine mkoani humo kufuata nyayo za GGML katika kuboresha mazingira ya kujisomea kwa wanafunzi.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong, alisema ni muhimu kuboresha mazingira ya utoaji elimu nchini ili kufikia lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

“Kutoa elimu bora kwa wote ni msingi wa kujenga dunia yenye amani na ustawi. Elimu huwapa watu maarifa na ujuzi wanaohitaji ili kuwa na afya njema, kupata ajira. GGML inafurahi kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,” alisema.

Akielezea malengo ya GGML katika kuboresha maisha ya Watanzania hususani kupitia uboreshaji wa sekta ya elimu, Strong alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka wa 2000, GGML imeendelea kuwekeza katika nyanja mbalimbali zinazoboresha maisha ya jamii nzima ya Geita na Tanzania kwa ujumla.

Alisema GGML imewekeza kwa kuzingatia masuala muhimu kama vile afya, elimu, maji, barabara na miradi ya kuzalisha kipato cha kaya na kukuza uchumi wa Taifa.

“GGML imewekeza katika utekelezaji wa miradi endelevu ambayo inainufaisha jamii inayouzunguka mgodi. Kwa hiyo mchango huu wa madawati unadhihirisha jukumu la GGML kama mwananchi anayehitaji elimu bora kubadilisha maisha yake,” alisema na kuongeza;

“Juhudi za GGML kujitolea kutekeleza miradi mbalimbali zinaendelea kuacha alama isiyofutika na kusaidia kuboresha maisha ya jamii kupitia uwepo wa kampuni hii mkoani Geita,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!