Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Nape ataka mifumo ya taarifa za hospitali iunganishwe
Afya

Nape ataka mifumo ya taarifa za hospitali iunganishwe

Nape Nnauye
Spread the love

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hospitali zimekuwa na mifumo mingi ambayo haisomani kiasi ambacho imechangia kuongezeka kwa gharama za matibabu kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri Nape ameyasema hayo leo Jumamosi wakati akifunga maonesho ya tatu ya kidijitali ya Afya na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili katika kampasi ya Mloganzanziala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufunga mafunzo hayo, Nape amesema maonesho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kujadili namna TEHAMA inavyoweza kuboresha huduma za Afya.

“Tunataka kwa kupitia TEHAMA tuboreshe huduma hiyo ili mtu akienda kokote taarifa zake ziwepo,” amesema Waziri Nape.

Nape ameeleza jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali ya katika kufanya mifumo ya TEHAMA isomane ili kuweza kupunguza gharama kubwa ya matibabu kwa wananchi pamoja na zile za uendeshaji.

Pia amesema kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano ambao ndio njia kuu ya kupeleka taarifa na kuna mifumo kadhaa lazima itengenezwe ili taarifa ziwe pekee kwa kila mtu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

Afya

573 wafariki kwa kipindupindu

Spread the loveTakriban watu 573 kati ya 11,640 walioambukizwa kipindupindu nchini Nigeria...

error: Content is protected !!