Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Weah rais wa kwanza kushindwa uchaguzi Liberia
Habari za SiasaKimataifa

Weah rais wa kwanza kushindwa uchaguzi Liberia

Spread the love

KIONGOZI anayeondoka madarakani nchini Liberia, George Weah, anaweka historia nchini humo kwa kuwa rais wa kwanza kushindwa katika kinyang’anyiro cha kuwania muhula wa pili madarakani. Inaripoti mitandao ya kijamii…(endeelea).

Weah ambaye alijizolea umaarufu mkubwa nchini mwake na duniani kwa ujumla wake kwa kucheza soka katika ngazi za juu zaidi kimataifa aliingia madarakani mwaka 2018 kwa muhula wa kwanza na alikuwa akitaraji kuendelea na awamu ya pili mwaka huu kabla ya kubwagwa na mpinzani wake Joseph Bokai katika uchaguzi wa marudio uliofanyika wiki iliyopita.

Bokai amepata ushindi mwembamba wa asilimia 50.89 ya kura dhidi ya asilimia 49.11 alizopata Weah. Ikiwa takriban kura zote zimeshahesabiwa, Bokai amemzidi Weah kwa takribani kura 28,000. Takwimu hizi zinaonesha ni kwa namna gani mchuano baina ya wawili hao ulivyokuwa mkali.

Kwa upande wa Bokai ushindi wake pia umeweka historia nchini humo kwa kuwa mtu wa pili kukirudisha chama tawala cha zamani madarakani. Na kwa Bokai binafsi ushindi wake ni kisasi dhidi ya Weah ambaye alimshinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2017.

Weah sasa anatarajiwa kuondoka madarakani mwezi Januari baada ya kuapishwa kwa rais mteule Bokai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!