Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto alia hujuma kambi ya wakimbizi Nduta kufungwa, adai inakwamisha maendeleo
Habari za Siasa

Zitto alia hujuma kambi ya wakimbizi Nduta kufungwa, adai inakwamisha maendeleo

Spread the love

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nduta iliyopo Kibondo mkoani Kigoma kufungua kambi hiyo ili wananchi wa wilaya hiyo wafanye biashara pamoja na wakimbizi ili kukuza uchumi wa eneo hilo kwa pamoja. Anaripoti Faki Sosi, Kigoma …(endelea)

Ameeleza kwamba kitendo cha kufungwa kwa kambi hizo ni moja ya vikwazo vya kukua kwa uchumi na maendeleo katika maeneo ya Kibondo.

Zitto ametoa wito huo jana alipokuwa akihutubia wananchi wa Jimbo la Muhambwe Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma katika ziara yake mkoani humo inayolenga kuzungumza na viongozi wa chama na wananchi.

Zitto alisema mkoa wa Kigoma umekuwa ukipokea wakimbizi tangu mwaka 1972, licha ya uwekezaji mkubwa wa Jumuiya ya kimataifa, watu wa Kigoma wamekuwa wanalalamika kuwa ukarimu wao hauwapi faida.

Alisema suala la kufungwa kwa kambi za wakimbizi Kibondo atalibeba kwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ili lishughulikiwa kwa haraka.

“Sera ya wakimbizi ni ile ile inayotumika Nyarugusi, Kasulu na Kibondo sasa iweje Kasulu waruhusiwe Kibondo wafungiwe kama sio hujuma, mkuu wa kambi Kibondo aache uchumi ushamiri… aache kufunga makambi” alisema.

Akizungumzia ubovu wa soko maarufu la samaki ambalo wafanyabiashara wengi wanauza bidhaa zao hapo ikiwemo mbogamboga na samaki alisema atatafuta wafadhili kwa ajili ya uboreshaji.

Alisema miundombinu ya soko hilo ni mibovu na wakati wa mvua wafanyabiashara wanafanya shughuli zao katika mazingira magumu huku Halmashauri ikiendelea kuwa kimya katika maboresho yake.

Katika mpango wa pili wa Kigoma Joint Program unaofadhiliwa na mashirika ya kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa, wametenga Sh. 220 bilioni kutatua vikwazo vya maendeleo ya Kigoma, bila ya kufungamanisha wakimbizi na uchumi wa Kibondo.

Mwenyekiti wa Jimbo la Muhambwe, Nicolaus Kilunga alieleza kero iliyopo baina ya wananchi na Idara ya Uhamiaji kwa kuzuiwa raia wa Burundi kuingia katika Wilaya hiyo na kufanya shughuli za kilimo.

“Utaratibu mbovu wa Idara ya Uhamiaji kuwapata warundi umesababisha baadhi ya wananchi kukwama kulima mashamba yao na wengine kushindwa kupanda mazao kwa wakati.

Kibondo tumekuwa tukiwategemea sana hawa Warundi kwenye kulima mashamba na kuwezesha mavuno mengi lakini utaratibu uliopo sasa una hatari ya baadhi ya wananchi kukumbwa na njaa” alisema.

Aidha, Kilunga alieleza adha wanayokutana nayo wananchi  wa Kibondo wakati wa kusafiri mara kwa mara kwenye mageti ya ukaguzi wakitakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!