Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli
Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the love

Mtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi amesema baba yao alikuwa mwanademokrasia wa kweli lakini pia hakuwa akitishika na mawazo mbadala. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema hivi sasa kuna baadhi ya viongozi wanaiimba demokrasia kwa nadharia lakini ndani ya nafsi yake Mzee Mwinyi alikuwa mdemokrasia wa kweli na wala hatishwi na maoni mbadala na ya kwake.

Abdullah amesema hayo leo Jumamosi wakati akitoa shukrani katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar kulipofanyika shughuli ya kuaga mwili wa baba yao aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024.

“Leo ni siku nzito sana kwetu, tumefikwa na msiba mzito lakini sisi sote kwa Mwenyezi Mungu tutarejea. Roho zetu zina huzuni, na macho yetu yana machozi kwa kumpoteza baba yetu, babu yetu, rafiki yetu lakini yote haya ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na safari yetu ni hukohuko.

“Tumesikia wakimzungumzia na amewagusa watu wengi lakini utu wake unaweza kupimika ukimtizama kama baba, mume, mwalimu na kama kiongozi. Hajabadilika katika kazi zake za kiuongozi, ni mwalimu wa kujitolea kuhakikisha wanafunzi wake wanamuelewa. Alikuwa kiongozi wa haki, mkweli, jasiri,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!