Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mwanafunzi aliyeacha shule kwa kukosa fedha za chakula arejeshwa
Elimu

Mwanafunzi aliyeacha shule kwa kukosa fedha za chakula arejeshwa

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya lleje, Farida Mgomi kwa kushirikiana na wazazi wamefanikiwa kumrejesha shuleni, Irene Mwazembe (15), mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya wasichana Ileje.

Mwanafunzi huyo alikatisha masomo na kwenda kufanya kazi za ndani katika Mji wa Tunduma baada ya wazazi wake kudaiwa kushindwa kumudu kuchangia gharama za chakula. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe. ..(endelea).

Hatua ya Irene kurejeshwa shuleni hapo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael kumuagiza mkuu wa wilaya hiyo, kuhakikisha anamrejeaha shuleni mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza ili aendelee na masomo.

Mbali na Irene, pia Dk. Francis ameagiza kurejeshwa shuleni hapo kwa wanafunzi wengine watatu ambao wazazi wao waliwahamisha na kuwapeleka katika shule za kutwa kwa kisingizio cha wazazi kukosa michango ya chakula.

Akimkabidhi mwafunzi huyo leo tarehe 21 Novemba 2023 kwa uongozi wa shule mbele ya mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mgomi alisema jitihada za kumrejesha shule mwanafunzi huyo zimetokana na wazazi kukubali na kutoa ushirikiano kwake.

“Mkuu wa mkoa kurejea kwa mwanafunzi huyu ni faraja kwa uongozi wa wilaya kwani lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata haki ya msingi ya kusoma kwani lengo la kuanzishwa kwa shule ya wasichana wilaya ya Ileje ilikuwa ni kuwakomboa watoto wakike” alisema Mgomi.

Kuhusu wanafunzi wengine waliondolewa shuleni hapo Magomi amesema jitihada za wanafunzi hao kurejeshwa shuleni hapo zinaendelea.

Kuhusu mwanafunzi wa tatu, amesema alihamishiwa mkoani Morogoro ambako anaendelea vizuri na masomo baada ya kuchukuliwa na baba yake mdogo.

Pamoja na jitihada hizo, Dk. Francis ametoa maelekezo kwa ofisa elimu wa mkoa huo Michali Lugola kutembelea shule zote za bweni za wasichana ili kubaini wanafunzi walioacha shule kwa kukosa fedha za chakula ili wawarejeshe kama ilivyofanyika katika shule ya wasichana Ileje.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Sharon Kadinde shule hiyo ya wasichana iliyoanzishwa mwaka huu ilipangiwa wanafunzi 75,  lakini walioripoti shuleni hapo ni 71.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!