Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro
ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the love

Mwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa kutekeleza maelekezo halali ya viongozi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa za kusimamishwa kwa Maganga ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), zimetolewa jana Alhamisi kupitia barua ya taarifa kwa umma iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Manispaa ya Temeke, Fransisca Mselemo.

 

Leah Ulaya, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

Barua hiyo imeeleza kuwa, Maganga amesimamishwa kazi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya chini ya Tume ya Utumishi wa Walimu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya nidhamu ya walimu.

Taarifa hiyo imeeleza uamuzi wa kusimamishwa kazi Maganga, ulifikiwa tarehe 5 Desemba 2023 ambapo kabla ya kusimamishwa, Maganga alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika iliyopo jijini Dar es Salaam.

Awali, Maganga aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na Rais Samia Suluhu Hassan ingawa ilielezwa kwamba hakuitikia uteuzi huo na kuendelea kusalia kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Pia hayo yanajiri wakati Katibu Mkuu huyo wa CWT na Rais wake, Leah Ulaya wakituhumiwa kutumia zaidi ya Sh bilioni saba katika maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za siku ya Mwalimu Duniani pamoja na kumbukizi ya miaka 30 ya CWT yaliyopangwa kufanyika kitaifa tarehe 13 Disemba mwaka huu mkoani Mwanza.

Baadhi ya wanachama wa CWT wamepinga matumizi hayo makubwa ya fedha huku wengine wakienda mbali zaidi na kuwatuhumu viongozi hao kuchochea migogoro ndani ya chama hicho kiasi cha kusababisha baadhi ya wanachama kujiengua na kujiunga na vyama vingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

error: Content is protected !!