Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo
Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the love

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika Gridi Taifa leo tarehe 8 Disemba 2023 majira ya saa 04:14 asubuhi, ndiyo iliyosababisha mikoa inayopata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa ikiwamo Dar es Salaam kukosa umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi TANESCO, imedai kuwa hitilafu hiyo imetokana na kusombwa na maji nguzo kubwa za kusafirisha umeme kutoka katika Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III eneo la Mto Gide, Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.

“Umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo,” imesema.

Aidha, jitihadi nyingine zinazofanywa na Shirika ni kuhakikisha miundombinu iliyoharibika inajengwa ndani ya muda mfupi, kuruhusu kusafirisha umeme unaokosekana katika Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III.

“Shirika linawaomba radhi kwa kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa umeme kwa kadri hali itavyozidi kuimarika,” imesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!