WANANCHI wa Musoma Vijijini, mkoani Mara, wameahidi kujenga shule ya sekondari itakayopewa jina la Prof. David Masamba, ili kuuenzi mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili kupitia machapisho mbalimbali aliyoyaandika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).
Ahadi hiyo imetolewa jana tarehe 31 Agosti 2023 na wananchi hao, katika mazishi ya Prof. Massamba, yaliyofanyika kijijini kwao Kurwaki, mkoani Mara.

Akizungumza katika ibada ya mazishi ya Prof. Massamba, Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, alisema wananchi wamekubali kujenga shule hiyo kijijini Kurwaki, ambako alizaliwa nguli huyo wa Kiswahili, katika eneo la Fonolojia ya Kibantu.
Prof. Muhongo alisema ujenzi wa sekondari hiyo utaanza Septemba 2023.
“Hapa tusitegemee kwanza fedha ya Serikali, tuanze tukijua Serikali inaweza ikatupatia au isitupatie lakini tuanze. Kwa hiyo hili jambo ni jipya sijawahi kusikia Kurwaki wanajitolea, kumbe wanamheshimu sana Massamba,” alisema Prof. Muhongo na kuongeza:
“Kwa kazi alizofanya huyu, vitabu alivyoandika huyu kikao chetu kinaazimia na kinapitisha jina la sekondari litakuwa Prof. Massamba. Hivyo tunajenga sekondari kwa heshima ya ndugu yetu sababu kazi alizofanya hatuwezi tukamzika akapotea hivi hivi.”
Leave a comment