Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amkabidhi Mchengerwa kivumbi uchaguzi Serikali za mitaa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia amkabidhi Mchengerwa kivumbi uchaguzi Serikali za mitaa

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameeleza kufurahishwa na uchapakazi wa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa ambaye sasa amehamishiwa katika Wizara ya Tamisemi kwa kuwa wizara zote alizowahi kuhudumu amegeuka kuwa bingwa wa mageuzi. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Aidha, amesema amemhamishia katika Wizara hiyo ya TAMISEMI kwa kuwa mwaka kesho kutakuwa na kivumbi (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa) ambacho anaamini ana kifua na atakimudu vizuri.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Septemba 2023 Visiwani Zanzibar katika hafla ya kuwaapisha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na viongozi wengine wa Serikali aliowateua juzi.

Pamoja na mambo mengine amewaasa viongozi wote aliowateua kuwa kwa sasa Serikali pamoja na wananchi wote kwa ujumla wanachohitaji ni mabadiliko katika utendaji ili kuleta maendeleo.

“Makamu wa Rais amelisema vizuri sana ni kuhusu ‘Reform’ yaani mabadiliko, tunachotaka ni mabdiliko, tunayoahidi watu kila wakati, tunaahidi mambo mengi ili kuwaletea maendeleo, twendeni tukadilike,” amesema Rais Samia.

“Nitakapowachambua hapa nitawaambia mabingwa wa reforms, na pengine nimseme mmoja hapa, Mchengerwa kwa mfano nilipompeleka utumishi mwanzo namteua akaingia kwa kasi hadi kelele zikawa nyingi, nikasema labda Waziri wangu kazidi kapandisha mabega.

“Nikasema labda nimpeleke michezo, akaenda michezo kazi aliyofanya ninyi wenyewe mmeiona, kaacha kazi nzuri sana. Katoka michezo nimempeleka utalii… mipango aliyoiweka sekta ile, Angela (Kairuki), ukienda ukifuata yaliyowekwa utalii inakwenda kupanda juu.

“Hassan (Abbas) yuko pale mzuri sana amefanya kazi nzuri sana na Waziri, wamekutana na Waziri (Mchengerwa) wameweka mipango mizuri sana, kwako ni kusimamia utendaji. Yatekelezwe yale ambayo yamewekwa tupandishe sekta yetu ya utalii,” ameongeza Samia

Hata hivyo, Rais Samia amemtaka Mchengerwa akafanye kazi ile ile aliyowahi kuifanya katika wizara alizowahi kuhudumu katika wizara zingine.

“Sasa nimempeleka (Mchengerwa) Tamisemi, mwakani kuna kivumbi na mimi nakujua najua unaweza, kivumbi kile kinafafanana na kifua chako najua unaweza kwa hiyo nimekupeleka Tamisemi ni kazi kazi ili mwakani tupite vizuri,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!