Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Biashara MC ajenga ukumbi wa bilioni 1.5, vijana wapewa ujumbe
Biashara

MC ajenga ukumbi wa bilioni 1.5, vijana wapewa ujumbe

Spread the love

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) jijini Dodoma, Wisdom Gowele ametoa wito kwa vijana kutumia nguvu zao ujanani kuwekeza katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo badala ya kuendekeza starehe na uzeeni kuishia kuwa ombaomba. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Mchungaji huyo wa Ilazo, ametoa wito huo jana Alhamisi jijini Dodoma katika ibada maalumu ya kuweka wakfu ukumbi wa mikutano uliojengwa na mshereheshaji maarufu jijini hapa, Mc John Mwangata  kwa gharama ya zaidi ya Sh 1.5 bilioni.

Meneja wa ukumbi wa Mwangata social Mc.John Mwangata.

Ukumbi huo wenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 600 umejengwa katika eneo la Maungu karibu na Mnada mpya wa Nkuhungu barabara ya Singida kilometa tisa kutoka mjini Dodoma.

Mchungaji Gowele amesema vijana wengi wamekuwa wakipambana kutafuta hela lakini wengi hujikita zaidi katika masuala ya anasa badala ya kuwekeza katika masuala ya kimaendeleo.

“Vijana mnatakiwa kujua kuwa kazi zinakuja na kuisha, ujana pia ni maji ya moto na kuna wakati wa kufanya kazi ukiwa na nguvu hivyo vijana nataka kuwaambia kuwa mnatakiwa kuwekeza miradi mikubwa mkiwa na nguvu.

“Fanyeni uwekezaji hususani kwa kutumia fursa zilizopo katika makao makuu ya nchi na mkiwekeza mtasaidia kuongeza pato la taifa, mtu binafsi pamoja na jamii kwa ujumla wake jambo ambalo litawafanya waliowengi kuondokana kukaa vijiweni” ameeleza Mchungaji Gowele.

Mchungaji Wisdom Gowele

Kwa upande wake Mwekezaji wa Ukumbi wa mikutano wa Mwangata social Hall, Mc John Mwangata aliwasihi wasanii pamoja na washereheshaji wenzie nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kula ‘bata’ badala yake wafanye shughuli zao kwa kuamini kuwa wanachokifanya ni sehemu ya ajira yao.

Amesema ameamua kufanya uwekezaji huo ikiwa ni sehemu ya kuweka alama ya kazi yake ya ushereheshaji.

“Kazi ya ushereheshaji ni kazi yenye kipato kidogo lakini ukijipanga unaweza kufanya kitu cha maana nimeamua kuwekeza katika ukumbi wa mikutano na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuwa iwapo nitakuwa nimeachana na shughuli hiyo nitakuwa na sehemu ya kujishikiza na kujipatia kipato.

“Najua kuwa uwekezaji huu ni mkubwa kwani mpaka nakamilisha nimetumia zaidi ya Sh. 1.5 bilioni na una uwezo wa kuchukua watu 600 kwa wakati mmoja jambo ambalo naweza kujivunia katika kazi zangu za ushereheshaji ndani ya miaka 20” amesema Mc Mwangata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Mwezi wa kutoboa ni huu, cheza Keno Bonanza utusue Maisha

Spread the love MWEZI wa Oktoba wengi hupenda kuuita mwezi wakutoboa wakiwa...

Biashara

Wataalam Uganda wapewa darasa teknolojia mpya uchimbaji madini katika maonesho Geita

Spread the loveMAONESHO ya Teknolojia ya Madini yamezidi kuwa darasa kwa wadau...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!