May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Museveni akemea mapinduzi Burkina Faso

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

Spread the love

 

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ameshutumu vikali mapinduzi yaliyotekelezwa nchini Burkina Faso dhidi ya serikali ya Rais wan chi hiyo, Roch Marc Christian Kabore. Anaripoti Mwandishi … (endelea).

Rais Museveni ametoa kauli hiyo jana tarehe 26 Januari, 2022 jijini Kampala nchini Uganda katika hafla ya kuadhimisha miaka 36 tangu atwae hatamu za uongozi nchini Uganda.

Amesema nchi za Afrika ya Magharibi zinatakiwa kujifunza kutoka kwake kuhusu namna ya kuzima wanaopanga mapinduzi.

“Baadhi ya viongozi wengi wa kiraia wanashindwa kuunda jeshi thabiti hivyo wanakuwa katika hatari ya kupinduliwa.

“Ndani ya miaka 10 iliyopita, takribani nchi 10 zimepinduliwa katika eneo la Afrika ya Magharibi. Hatufai kuruhusu hili kufanyika. Hao wanajeshi wanapofanya mapinduzi hawaulizwi chochote na raia kwa sababu hawakuchaguliwa,” amesema.

Amesema vuguvugu la mapinduzi katika nchi za Afrika Magharibi lilianza baada ya Serikali ya Muammar Gaddafi nchini Libya kuangushwa kisha kuzalisha magaidi wengi.

Amesema makundi hayo ya kigaidi yamesambaa katika nchi za Mali, Niger, Guinea, Burkina Faso na nchi nyingine za Afrika.

error: Content is protected !!