May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Familia ya Mrisho yaomba zuio umilikishwaji kiwanja

Wajane na watoto wa Marehemu Mzee Amir Mrisho, wakiwa nje ya Mahakama ya Mwanzo Upanga, Ilala jijini Dar es Salaam

Spread the love

 

WATOTO wa marehemu Mzee Amir Mrisho, wamepeleka maombi ya kuzuia mchakato wowote wa umilikishwaji wa Kiwanja namba 108 Port Access kilichopo wilayani Temeke kwa mtu yoyote  hadi kesi za msingi itakasikilizwa. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Kiwanja hicho ni sehemu ya mirathi namba 167 ya mwaka 2006 ambayo inatambua wasimamizi wa mirathi wanne wa familia ya Mzee Mrisho ambao ni Sophia, Omar, Hadija na Mrisho.

Moambi hayo yamewasilishwa katika Makahama ya Mwanzo Upanga, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi, Julieth Dama ambaye amesema leo atatoa uamuzi kuhusu ombi hilo.

Akizungumza baada ya Hakimu Mkazi, Dama kuhairisha shauri hilo hadi leo, Wakili Msomi Gabriel Masinga alisema walalamikaji wamelazimika kupeleka maombi hayo, kutokana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupitia Kamshina wa Ardhi kutoa notisi ya kumilikisha eneo hilo kwa Kampuni na Nahla.

Masinga alisema iwapo mchakato wa umilikishwaji utafanyika kama notisi ilivyotolewa  ni dhahiri kuwa kesi ya msingi iliyofunguliwa na wanufaika na mirathi hiyo haitakuwa na mashiko.

“Hapa kuna kesi ambayo inapinga uuzwaji wa eneo hilo la kiwanja namba 108, hivyo iwapo tutaruhusu notisi ambayo imetolewa kufanya kazi ni dhahiri kuwa kesi ya msingi haitakuwa na mashiko, imani yetu leo hakimu atatoa zuio, ili haki itendeke,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya familia Mtoto wa Marehemu Mzee Mrisho, Abdul Mrisho alisema kadhia wanayopitia inatokana na dada yao Sophia Mrisho ambaye wadai kuwa amewazunguka ndugu yake.

Abdul alitoa ombi la Rais Samia, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Anjelina Mabula kuwasaidia kwa kuwa wanaona mahakama zimeshindwa.

“Huu ni mwaka wa 15 tunahangaika mahakamani, kila tukiangalia tunaona dalili za rushwa, tunaomba Rais Samia na viongozi wengine watusaidie, kuna wajane watatu katika kadhia hii na watoto 21 tunaomba sana haki itendeke,” alisema.

Wanufaika wa mirathi hiyo ni Aseline, Amina  na Husna ambao ni wajane wa marehemu Mrisho.

Wengine ni watoto wa marehemu Mzee Mrisho ambao ni Omari, Naima, Mariam, Rachel, Rehema, Mrisho, Juma, Zahara, Zainabu, Sharifa, Saidi, Karim, Rajab, Abdul, Hadija, Sauda, Hussein, Ibrahim, Iddi, Riziki  na Sofia.

error: Content is protected !!