December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtandao wa Jamii forum imesajiliwa: Shahidi

Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums

Spread the love

MKUREGENZI mtendaji wa Usajili wa Vikoa vya Mitando Nchini (TZNIC), Abibu Mtahigie amekiri kuwa mtandao wa Jamii Forum umesajiliwa kwa kikoa cha Tanzania (Tz) anaandika Faki Sosi.

Akitoa ushahidi kwenye Mahakma ya Hakimu Mkazi Kisutu leo amedai kuwa mtandao huo wa Jamii Forum umesajiliwa kwa vikoa viwili ambavyo havijaanza kutumika.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa anayesikiliza ushahidi huo ambapo upande wa utetezi uliwakilishwa na Peter Kibatala , Mutabesya na Jebra Kambole huku Kishenyi Mutalemwa akisimama upande wa Jamhuri.

Shahidi alipokuwa akijibu maswali ya mawakili wa utetezi kuhusu kusajiliwa kwa kikoa cha Jamii Forum alijibu kuwa kimesajiliwa tarehe 28 Novemba Mwaka 2009, lakini amesema bado haijaanza kufanya kazi.

Kesi hiyo imeahirishwa kwa ajili ya kuendelea na mapitio ya ushahidi huo kwa upande wa Jamhuri itatajwa tena Tarehe 17 Oktoba Mwaka huu.

error: Content is protected !!