Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili avipa maagizo vyama vya siasa
Habari za Siasa

Msajili avipa maagizo vyama vya siasa

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sixty Nyahoza,
Spread the love

 

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, imevitaka vyama vya siasa kuanza kuboresha mifumo yao ya  ndani ya  demokrasia kabla havijatoka nje. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …  (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022 na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha ACT-Wazalendo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo mkuu unalenga kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Makamu Mwenyikiti Bara.

Nyahoza amevishauri vyama hivyo kuenzi misingi ya demokrasia kwa kubadilisha viongozi.

“vyama vyote viweze kudumisha na kuboresha suala la demokrasia sababu hatujafikia mwisho, bado tuna changamoto ya demokrasia ndani ya vyama. Unajua msingi mkubwa kwenye vyama ni demokrasia, uchaguzi ni suala ambalo linaanzia ndani,” amesema Nyahoza.

Nyahoza amesisitiza “vyama vya siasa muanzie ndani ya vyama. Tujitahidi kuboresha ndani ya chama ikishakuwa vizuri, nje ya chama itakuwa mwisho. Demomrasia ndani ya chama ikiwa changa hata nje itakuwa changa sababu watu hutoka huko wanaenda kule. Tunaviasa vyama vya sissa hili suala tuendelee kulirekebisha.”

Nyahoza amekipongeza chama cha ACT-Wazalendo kwa uamuzi wake wa kujaza mapema nafasi ya Maalim Seif, aliyefariki dunia tarehe 17 Februari 2021 kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Tulipata tatizo kubwa kama nchi, halikuwa lenu peke yenu kwa kuondokewa na Maalim Seif  mkapata uwazi pale, kwa vyama sisi tunaelewa kwa taarifa za vyama kuna vyama vingine mtu anakaimu miaka minne, mnaanza kusuguana mbona nafasi iko wazi. Nyinyi kwa matashi yenu mkaamua kuingia gharama kuitisha mkutano kujaza nafasi,” amesema Nyahoza.

Aidha, Nyahoza amevishauri vyama vya siasa kuiga mfano wa ACT-Wazalendo, kufanya mdahalo wa kuwapima wagombea wake katika nafasi mbalimbali za uongozi.

” Mnajaza nafasi za uongozi kwa misingi ya kidemokrasia na kisheria, jana kulikuwa na mdahalo sisi tunapongeza sana kuwa na mdhahalo sababu sijaiona kwa vyama vingine,” amesema Nyahoza na kuomgeza:

“Sio lazima kila mtu aige ile staili ina uzuri wake inaonyesha uwazi, ushindani ulipo kisiasa na ustaarabu watu kuonesha mawazo tofauti halafu mwisho wa siku kuchagua. Hii inaondoa attention kufikia uchaguzi.”

Jana Jumamosi, ACT-Wazalendo kilifanya mdahalo wa kuwapima wagombea waliopitishwa na Halmashauri kuu yake kugombea nafasi ya Maalim Seif, ambao ni Juma Duni Haji na Hamad Masoud Hamad.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!