Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Prof. Mkumbo achochea ufaulu wa hisabati Ubungo, Waziri Mkenda atoa tuzo
Elimu

Prof. Mkumbo achochea ufaulu wa hisabati Ubungo, Waziri Mkenda atoa tuzo

Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amekabidhi tuzo kwa Walimu ambao wanafunzi wao wamefanya vizuri katika somo la Hisabati kwenye Mtihani wa Kidato cha nne katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Kitila Mkumbo, zimetolewa leo Jumamosi tarehe 29 Januari 2022, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Prof. Mkenda, amesema Serikali inafanya utafiti ili kujua sababu za wanafunzi kufanya vibaya katika somo la Hisabati Kidato cha nne 2021.

 

Prof. Mkenda amesema kwa mwaka 2021 hali ya ufaulu kwa somo la Hisabati kidato cha nne ni mbaya hali iliyolazimu kufanyika kwa utafiti ili kujua sababu za wanafunzi kutokufanya vizuri.

“Ufaulu wa somo la Hisabati ni janga, tunapaswa kulikazania na kwa nchi nzima Wanafunzi wamefaulu kwa asilimia 19.45 kiwango ambacho hakiridhishi na kwa Ubungo ufaulu ni asilimia 16 hali inayoonyesha kuchochewa na Tuzo za Mbunge Prof. Kitila Mkumbo zinazofahamika kama KiuHisabati” amesema Profesa Mkenda.

Waziri huyo amempongeza Profesa Mkumbo kwa kuandaa tuzo za KiuHisabati kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwa somo la Hisabati kidato cha nne mwaka 2021 jambo ambalo limeongeza ufaulu wilayani humo

“Tunafanya utafiti ili tuweze kufahamu chanzo cha Wanafunzi kutokufanya vizuri kwenye somo la Hisabati na tunakusanya taarifa kwa kila shule jambo ambalo litatusaidia kupata suluhisho,” amesema Profesa Mkenda

Kwa upande wake, Profesa Mkumbo amesema ameanzisha programu ya KiuHisabati ili kuchochea ari ya walimu kufundisha somo hilo na Wanafunzi kujifunza wakijua kuwa ipo motisha kwao pindi wanapofanya vizuri hali ambayo imeifanya Wilaya ya Ubungo kufanya vizuri mwaka 2021.

Prof. Kitila amesema katika tuzo hizo walimu ambao wanafunzi wao wamefanya vizuri katika somo la Hisabati kidato cha nne mwaka 2021 wamepatiwa Sh. 100,000 kwa kila mwanafunzi aliyepata Alama A.

Mbali na Motisha hiyo kwa walimu, Profesa Mkumbo amesema atawalipia ada ya masomo ya Kidato cha tano na sita wanafunzi wote waliopata alama A kwa somo la Hisabati huku waliopata alama B wakilipiwa nusu ya ada kwa kidato cha tano na sita.

“Licha ya kutoa motisha hiyo ya Sh. 100,000 kwa waimu wa hisabati kwa kila mwanafunzi aliyefanya vizuri, Wakuu wa Shule wa Shule zote zilizopata alama A nao watapatiwa kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja” amesema Profesa Mkumbo

“Wanafunzi wote waliopata alama A, B na C katika matokeo ya Kidato cha IV mwaka 2021 nitawapeleka kufanya utalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa siku 3 pamoja na Walimu wao ili kuwahamasisha na wengine kufanya vizuri” amesema Profesa Mkumbo

Prof. Kitila Mkumbo amesema tuzo hizo zimekuwa chachu kwa Wanafunzi na walimu maana ufaulu kwa Wilaya ya Ubungo umeongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 2020 na kufikia asilimia 16 mwaka 2021.

Amesema, mwaka 2020 hakuna mwanafunzi aliyepata alama A lakini kuanzishwa kwa programu hiyo imefanya wanafunzi 30 kupata A huku B zikiongezeka kutoka tisa hadi 31.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James amesema ukizungumzia uimara wa masomo yote msingi wake ni Hisabati na pale mwanafunzi anapofanya vizuri kwenye Hisabati na masomo mengine anafanya vizuri pia.

Amesema Wananchi wa Ubungo wanayo bahati ya kupata Mbunge anayejali suala la Elimu jambo litakaloifanya Wilaya hiyo iendelee kufanya vizuri kielimu.

Amesema uongozi wa Wilaya unaunga mkono kazi inayofanywa na Prof. Kitila Mkumbo katika kuinua Elimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!