Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina aanza na unyang’anyi wa mifugo bungeni
Habari za Siasa

Mpina aanza na unyang’anyi wa mifugo bungeni

Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luhaga Mpina
Spread the love

MBUNGE wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, ameihoji Serikali itatekeleza lini amri za mahakama za zinazoielekeza kurudisha mifugo ya wananchi iliyokamatwa katika hifadhi za wanyama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mpina amehoji hayo leo Ijumaa, tarehe 8 Aprili 2022, bungeni jijini Dodoma, ikiwa zimepita siku chache tangu aweke ahadi kwamba atalitumia Bunge la Bajeti, kutoa hoja ngumu za wananchi bila kuogopa vitisho.

“Je, ni lini Serikali itarejesha kwa wafugaji mifugo iliyokamatwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapoto Tanzania (TAWA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), ambayo mahakama ilitoa hukumu irejeshwe?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Marry Masanja, amesema kama kuna wananchi walioshinda kesi na mahakama kuamua warejeshewe mifugo yao, wawasilishe malalamiko yao wizarani ili yafanyiwe kazi.

Jibu hilo halikumridhisha Mpina, aliyedai waziri huyo amedanganya kwa kuwa orodha ya wananchi wenye mifugo iliyokamatwa iko wizarani.

“Swali ninalouliza hapa, orodha iko wizarani na waziri anayo hiyo orodha. Kwa nini anakwepa kuwalipa wafugaji wanyonge ambao wameshinda kesi mahakamani na kutudanganya hapa kwamba hiyo orodha hana?” amesema Mpina.

Masanja amelijibu swali hilo akisema wizara yake haijapata orodha hiyo na kuwataka wafugaji wenye mifugo hiyo kwenda wizarani ili wapate ufumbuzi wa malalamiko yao.

“Kama nilivyokuji kwenye swali la msingi kwamba, mpaka sasa hatujapata orodha ya wafugaji ambao wanalalamika hawajarudishiwa mifugo yao na kama nimeeleza kwamba, kesi inapolekekwa mahakamni sisi tunapeleka vielelezo lakini kesi inakuwa chini ya hakimu sisi tunakuwa mashahidi,” amesema Masanja na kuongeza:

“Endapo kuna mfugaji ana kesi inatudai wizara basi waje wizarani, tutakaa pamoja tuichambue hiyo kesi tutaweza kutekeleza kama Serikali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!