Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kimei aionya Serikali: Tufanye uchambuzi tusije kukopa ili tule
Habari za Siasa

Kimei aionya Serikali: Tufanye uchambuzi tusije kukopa ili tule

Mbunge wa Vunjo mkoani Kilimanjaro (CCM), Dk. Charles Kimei
Spread the love

MBUNGE wa Vunjo, Dk. Charles Kimei ameonya Serikali kuhusu ujenzi wa miundombinu ya kijamii bila kuangalia gharama za sasa za uendeshaji. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma…(endelea)

Kimei amtoa kauli hiyo leo Ijumaa ya tarehe 8 Aprili bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya Bajeti yaOfisi ya Waziri Mkuu.

Kimei amesema Serikali inapojenga shule lazima ifikiri OC na mishahara itakayoiwezesha ile shule ifanye vizuri.

“Hili ni suala ambalo nikiangalia najisikia kushrink sana nasema hivi iotakuja kufika mahali mahitaji yote ya ualimu na watoa huduma za afya na wote wakapewa kama inavyoombwa, naamini bajeti nzima isingetosha.

“Kwahiyo lazima tufanye uchambuzi vizuri tusije kufikia kukopa ili tule , na mimi nakubaliana na haya mambo ya mfumuko wa bei yanayoendelea,” amesema Kimei.

Amesema mfumuko wa bei umekuwa juu katika mataifa makubwa na kushauri kuwa kuna haja ya kubana matumizi.

Mtaalamu huyo wa masuala ya fedha, amesema mfumuko wa sasa hauwezi kudhibitiwa na Benki Kuu ya Tanzania kwasababu unasukumwa na mfumuko wa bei wa dunia ambapo amesema nchi kubwa kama Marekani umefikia hadi asilimia saba.

Amesema kutokana na hali hiyo kuna haja ya kubana matumizi kuanzia kwa Serikali hadi mtu binafsi.
“Lazima tujue mfumuko wa bei Marekani na ukanda wa Ulaya umefikia hadi asilimia saba kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa tangu mwaka 1982, kwahiyo hili ni suala la dunia hatuwezi kusema tunalidhibiti kwa kwenda kukopa ni wakati wa kukaza mikanda hakuna namna ya kuepuka hili, kama ulikuwa unaenda jimboni kila siku nenda mara mbili au tatu kwasababu hela utakayokuwa nayo haitatosha.

“Hili suala si la kwetu na sio jambo la haraka haraka na wala Benki Kuu haiwezi kulishughulikia is not monetary policy (sera ya fedha) ya hapa kwetu inaweza kulishughulikia kwasababu linakuwa driven (sukumwa)na import inflation (mfumuko wa nje) ”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!