Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kanali Simbakalia ashauri mashirika yaliyoanzishwa na Mwalimu Nyerere yaimarishwe
Habari za Siasa

Kanali Simbakalia ashauri mashirika yaliyoanzishwa na Mwalimu Nyerere yaimarishwe

Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia
Spread the love

 

KANALI Mstaafu, Joseph Simbakalia, ameshauri mashirika yaliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, kwa ajili ya kuchagiza maendeleo, yaimarishwe ili kuenzi maono yake ya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kanali Simbakalia ametoa ushauri huo leo Jumamosi, tarehe 9 Aprili 2022, katika mdahalo wa kitaifa wa kuadhimishwa miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere, uliofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, ametaja mashirika ambayo yanatakiwa yaimarishwe ikiwemo, Kituo cha Teknolojia ya Magari Tanzania (TACT)-Shirika la Nyumbu, Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).

“Zipo taasisi tano au sita za msingi kabisa, ambazo ningeshauri turudi nyuma kwa kutambua makubwa yaliyofanya. Tuone nini hayakupewa hayo mashirika, uwezo gani hayakupewa ili yahuishwe hatimaye kutupeleka kwenye maono ya Baba wa Taifa, aliyokuwa nayo,” amesema Kanali Simbakalia.

Katika hatua nyingine, Kanali Simbakalia ameshauri vyuo vikuu vianzishe mitaala ya kuwafundisha wanafunzi kuhusu masuala ya uchumi wa viwanda.

Aidha, Kanali Simbakalia, ameshauri muda wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), uongezwe ili kuwandaa vijana katika kufanya kazi katika uchumi.

“Nashauri na ingefaa tuangalie upya JKT ili muda wanaokaa uongezwe turudi kwenye utaratibu wetu wa miezi 18, hata zaidi kama mtu hakimbilii chuo kikuu. JKT iwe chuo kikuu cha stadi za maisha, kuwaandaa vjana kufanya kazi katika uchumi,” amesema Kanali Simbakalia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!