Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Montana mbioni kupiga marufuku matumizi ya ‘Tiktok’
Kimataifa

Montana mbioni kupiga marufuku matumizi ya ‘Tiktok’

Spread the love

 

JIMBO la Montana ya Marekani lipo Mbioni kupiga marufuku ya matumizi ya mtandao wa kijamii wa Kichana wa ‘TikTok.’ Gazeti la Montana Standard liliripoti … (endelea).

Alhamisi ya juma lililopita Bunge la Montana lilifanya mchakato wa kupiga kura ya maoni juu ya Tiktok watu 69 walipiga kura kuunga mkono kupigwa marufuku kwa mtandao huo huku 39 wakipinga.

Muswada wa Seneti 419 utapiga marufuku Aplikasheni ya AppStore ya kampuni ua simu ya Apple na Google kuweka Aplikesheni ya ‘Tiktok’ kwa watu wa Jimbo hilo ambapo imeelezwa kampuni itakayokiuka italipa maelfu ya dola kama Faini.

Mtazamo wa Bunge hilo linaloongozwa na chama cha Republican ni kwanba mtandao huo ni kama kivuli cha nchi ya China ambapo inaweza kuwa tishio kwa Marekani.

“Tunajua Jamhuri ya watu wa china ni mmoja wa wapinzani wetu wakuu, lakini tunawaruhusu kukusanya habari kwa uhuru kuhusu Montanans.” alinukuliwa Katie Sullivan, D-Missoula, Mmoja wa wakilishi wa bunge hilo.

Wakilishi wengine walitoa hoja kuwa Montana isiishie kuzuia mtandao huo pekee bali mtandao wowote wenye lengo la kuchimba taarifa .

Hapo awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok, Shou Zi Chew alitoa ushahidi mbele ya Bunge la Marekani huku kukiwa na ongezeko la wasiwasi wa usalama na uwezekano wa ushawishi wa serikali ya China juu ya kampuni hiyo.

Alikabiliwa na maswali makali kutoka kwa Kamati ya Nishati na Biashara ya Bunge la Merikani.

Mwanasheria wa Marekani Debbie Lesko wakati wa mahojiano yake alinukuu India na nchi nyingine ambazo hivi majuzi zimepiga marufuku TikTok .

“Hiki (TikTok) ni chombo ambacho hatimaye kiko chini ya udhibiti wa serikali ya China na kinapiga kelele kwa wasiwasi wa usalama wa kitaifa, nchi hizi zote na mkurugenzi wetu wa FBI wanawezaje kukosea? aliuliza Lesko.

Zi Chew alijibu kuwa anadhani kuwa hatari nyingi zilizoonyeshwa ni hatari za kidhahania na za kinadharia. sijaona ushahidi wowote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!