June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mke wa mtu sumu… denti afumaniwa, auawa

Spread the love

 

MWANAFUNZI mmoja wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kapsumbeiywo, huko Kuresoi Kusini, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya ameuawa baada ya kufumwa na mke wa mtu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Edmond Kipng’etich (19) aliyefumaniwa na Mume (35) wa mwanamke huyo,M aliuawa kwa kukatwakatwa vipande kwa panga.

Akithibitisha kisa hicho, Ofisa Upepelezi wa makosa ya jina katika wilaya hiyo ya Kuresoi, Peter Obonyo alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya Nakuru Level Five.

Alisema tayari polisi wameanzisha msako dhidi ya mshukiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Japheth Bii ambaye anasemekana aliingia mitini baada ya kutekeleza mauaji hayo ya kinyama.

error: Content is protected !!