Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Tangulizi Waandishi 59 wapenya tuzo za EJAT 2020
Tangulizi

Waandishi 59 wapenya tuzo za EJAT 2020

Dk. Joyce Bazira, Mwenyekiti wa Majaji wa Tuzo za EJAT
Spread the love

 

KAMATI ya maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) imesema jumla ya waandishi 59 wameteuliwa kuwania tuzo hizo kati ya waandishi 147 waliowasilisha kazi zao. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea0.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 1 Septemba, 2021 jijini Dar es Salaam, mmoja wa majaji wa tuzo hizo, Dk. Joyce Bazira amesema watueliwa kwa mwaka 2020 wapo katika makundi 19.

Amesema wateule hao wamepenya baada ya jopo la majaji lililokutana Bagamoyo kwa siku nane kuanzia Agosti 12 hadi 19 2021 kumaliza jukumu la kupitia kazi zilizowasilishwa kuwania tuzo hizo.

Amesema kati ya hao, 20 wanaandikia magazeti, 7 ,wanatoka katika mitandao ya kijamii (online) na kutoka Redio 20, na Runinga 13.

“Kati ya wateule hao wa EJAT 2020, 26 ni wanawake. 10 ni kutoka kwenye magazeti, wawili kutoka mitandao ya kijamii na 14 kutoka vyombo vya habari vya kielektroniki.

“Wanaume ni 33 ambapo 10 kati yako ni kutoka kwenye magazeti, 19 ni waandishi wa redio na runinga na watano wanaandikia mitandao ya kijamii (online media) wakati mmoja ametoka katika maeneo mawili,” amesema.

Amesema jopo la majaji liliongozwa na Dk. Joyce Bazira. Majaji wengine ni Bi Imane Duwe, ambaye alikuwa katibu wa jopo Bw. Mkumbwa Ally, Bw . Lucas Liganga, Bw Selemani Mpochi, Dk Egbert Mkoko na Bw. Ally Masoud.

Aidha, washindi wa tuzo hizo watajulikana rasmi katika kilele cha Tuzo za EJAT 2020 zitakazofanyika septemba 10, 2020 katika kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe Joseph Warioba.

Pia siku hiyo, mashindano ya EJAT 2021 yatazinduliwa huku kilele cha sherehe za Tuzo za mwaka 2020 kinatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana na tahadhari za ugonjwa wa UVIKO- 19.

“Moja ya masharti yake ni kuepuka mikusanyiko mikubwa. Kutokana na hali hiyo, wateule wote watatakiwa kutuma picha zao (passport size) za rangi kupitia barua pepeelizabeth@mct.or.tz na saumu@mct.or.tz ili kuwatambua wateule wakati wa sherehe

“Pia sherehe hizi zinafanyika kwa njia ya mtandao wateule pamoja na wadau mbalimbali watatumiwa link kwa ajli ya kujiunga na kutazama shughuli hizi moja kwa moja. Wadau wachache wataalikwa kuhudhuria kilele cha sherehe hizi,” amesema.

Amesema wateule katika tuzo za 2020 wametokana na jumla ya kazi 395 kutoka kwa waandishi wa habari nchi nzima zilipokelewa kwa ajili ya kushindanishwa katika makundi 19 ya tuzo hizi

“Katika mashindano ya mwaka huu, washiriki 77 walioleta kazi zao ni wanaume na 70 ni wanawake, ambapo jumla inafanya waandishi walioshiriki kuwa 147 kutoka vyombo mbalimbali vya habari bara na visiwani

“Kati ya kazi 395 zilizowasilishwa  59 ziliwasilishwa na waandishi wa habari kutoka Dar es salaam wakifuatiwa na waandishi wa habari kutoka kisiwa cha pemba ambao walileta kazi 27, Unguja kazi 24, mwanza kazi 22 na Dodoma kazi 21. Kazi zilizopokelewa zinatoka kwenye vyombo vya habari 72 vikiwemo vikubwa na vidogo kama radio za kijamii,” amesema.

Aidha, Dk Joyce Bazira ametoa baadhi ya vigezo muhimu vya kufuata ili kazi yako iweze kupita kwenye mashindano hayo.

Amesema; “kwenye magazeti vipo vigezo 10, kwenye Redio na Tv vipo vigezo 10 na Online tv pia wapo na vigezo vyao kwahiyo kila kazi ina vigezo vyake.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

Habari za SiasaTangulizi

Lema kurejea Machi 3 na sumu ya kuangamiza chawa

Spread the love  HATIMAYE Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia...

error: Content is protected !!