Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mil.75 za mfuko wa Jimbo kujenga maabara za Sekondari Musoma Vijijini
Habari za Siasa

Mil.75 za mfuko wa Jimbo kujenga maabara za Sekondari Musoma Vijijini

Prof. Sospeter Muhongo, Mbunge wa Musoma Vijijini
Spread the love

FEDHA za mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Tarime, kiasi Cha Sh.75 milioni, zinatarajiwa kujenga maabara ya masomo ya sayansi katika shule za sekondani jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Taarifa kuhusu mpango huo imetolewa  tarehe 21 Desemba 2022 na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo (CCM).

Taarifa ya ofisi hiyo imesema, fedha hizo zitasaidia kuongeza maabara katika shule za sekondari Kwa kuwa Hadi Sasa ni shule tatu kati ya 25 za Serikali, ndizo zenye maabara.

“Ni sekondari tatu tu zenye maabara ya masomo ya Physics, Chemistry na Biology, zilizokamilika na zinatumika ipasavyo. Sekondari nyingine zinatumia vyumba vya madarasa kuwa maabara zao zinapohitajika. Kwa hiyo Sh. 75 milioni za mfuko wa Jimbo zilizopokelewa hivi karibuni zitatimika kuchangia ujenzi wa maabara hizo tatu kwenye baadhi ya sekondari zetu,” imesema taarifa hiyo.

Ofisi hiyo imetoa with Kwa shule za sekondari zinazohitaji kuchangiwa vifaa vya ujenzi vya maabara, kutuma kaombi Yao Kwa Katibu wa Kamati ya Fedha za Mfuko wa Jimbo, kabla ya tarehe 10 Januari 2023.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Jimbo la Musoma Vijijini, lina kata 21 zenye shule za msingi 118, sekondari 27 na shikizi nne.

Ambapo baadhi ya kata zimeamua kujenga sekondari nyingine Ili kutatua matatizo ya umbali mrefu wa wanafunzi wanaotembea kwenda masomoni, pamoja na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.

Hadi sasa sekondari mpya Tano zimepangwa kujengwa jimboni humo ambapo ujenzi umeanza kwa baadhi ya kata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!