Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: JNHPP ulipitia vikwazo vingi lakini hatukurudi nyuma
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia: JNHPP ulipitia vikwazo vingi lakini hatukurudi nyuma

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP)ni ushahidi tosha kuwa Tanzania inaweza kufanya mambo yake bila kikwazo baada ya kupitia vikwazo vingi na kuvishinda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Rufiji, Pwani … (endelea). 

Rais Samia amesema kwa ujasiri wa wa mtangulizi wake Hayati Dk. John Magufuli waliamua kutekeleza miradi huo ikiwa ni fikra za Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Nakumbuka hujuma na vikwazo ambavyo vilitokea katika kuelekea utekelezaji, ila tulisema haturudi nyuma hadi mradi ukamilike,” amesema.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 22 Desemba, 2022, wakati wa zoezi la ujazaji wa maji wa bwawa hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 78 hadi sasa.

Aidha, Rais Samia amewataja watu wote ambao wameshiriki katika utekelezaji wa miradi huo na kuwataka waendelee uzalendo huo.

Amesema mchakato wa mradi ulianza 2017 ila rasmi utekelezaji ulianza 2018 ambapo hadi sasa mradi umefikia asilimia 78.6 hivyo ni matumaini yake kuwa utakamilika kwa wakati.


Amesema wakati anachukua nafasi ya urais alikuta mradi huo ukiwa asilimia 38 ila amejipanga kuusimamia na kuhakikisha unakamilika.

Amesema mradi huo utakuwa na faida nyingi kwa kuzalisha umeme, kukuza kilimo, utalii, kuondoa mafuriko na kutoa ajira za moja kwa moja.

Aidha ameitama wizara ya kilimo kusimamia kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Rufiji kwa kutenga maeneo makubwa ya kilimo na yale .

Amesema kuna hekta laki nne ambazo zikitumiwa vizuri zitawezesha kilimo kukua.

Amewataka wafanye mnada wa wazi wa mashamba katika eneo hilo ili kuvutia wawekezaji wakubwa wa kilimo.

Ameiagiza wizara ya uvuvi ije na mpango mahususi wa uvuvi ili kuwezesha wavuvi kuvua samaki katika eneo hilo.

Ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na TANROADS kuandaa mpango wa ujenzi wa barabara kutoka u
Utete hadi Chalinze.

Kwa upande wa Wizara ya Maji ameitaka ishirikiane na Dawasa kupeleka maji katika mji wa Mloka ili yaweze kwenda Dar es Salaam, huku ujenzi wa Bwawa la Kidunda likiendelea kujengwa.

Amesema pia mradi huo unahitajika kutumika kutunza na kulinda mazingira na misitu na kwamba kwa sasa ni suala la kufa na kupona.

Amewataka watu wa Iringa na Mbeya kuacha kuchepusha maji ili maji yaweze kujaa kama ambavyo inahitajika.

Pia Wakazi wa Iringa na Morogoro wametakiwa kuacha uharibifu wa mazingira ili maji kutoka Mto Kilombero na mingine.

Aidha, amewataka wakuu wa mikoa kuondoa mifugo ambayo imeingia katika mabonde na hifadhi kuondolewa kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Rais Samia amesema ng’ombe wanaoingizwa waondolewe bila kuogopa watu wakubwa.

Pia amesema wananchi wote ambao wapo karibu na mto Rufiji waondolewe ili kuhakikisha mto unakuwa salama.

Amewataka wasaidizi wake kusimamia mafunzo ya mazingira kwa wananchi wote ambao wapo karibu na vyanzo vya maji.

“Kauli mbiu ya bwao lako, langu na letu isimamiwe vizuri ili tuweze kunufaika na mradi huu wa kihistoria,”amesema.

1 Comment

  • Hongera mama.
    Peleka muswada wa sheria unaokataza watu na mifugo kwenye mito na mazingira yake.
    Halafu, wanasheria wa serikali watakuwa na sheria ya kutumia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!